Kamanda wa polisi wa
mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo . (picha na
Mwamvua Mwinyi)
……………………….
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi mkoani
Pwani ,limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto watatu akiwemo wa miezi kumi
,waliouawa kwa kunyweshwa sumu na baba yao
mzazi.
Chanzo cha kutenda kitendo
hicho cha kikatili kinadaiwa ni kutokana na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa
watoto hao.
Kamanda wa polisi mkoani
humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa alieleza tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia jana huko kata ya Kibindu, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
Aliwataja watoto hao kuwa
ni pamoja na Shaila Salehe miaka sita ,Nurdin Salehe (4)na Sabrat Salehe mwenye
miezi kumi waliouawa kwa kunyweshwa sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu
iitwayo Twiga Amine na baba yao mzazi Salehe Masokola (22),mkazi wa kijiji cha
Kunwe ,Mvomero mkoa wa Morogoro .
Wankyo alibainisha,baba wa
watoto hao alikuwa na mgogoro na mkewe ambae ndiye mama wa watoto .
“Mtuhumiwa alipowafuata
watoto kutoka kwa mama mkwe wake kwa madai kwamba anakwenda kucheza nao na
angewarudisha baadae ” alifafanua Wankyo.
Alielezea,mtuhumiwa
aliwapakia marehemu kwenye baiskeli kutoka Kunke hadi kitongoji cha Ditele
,Kibindu ambapo aliwanywesha dawa hiyo kwa kuwachanganyia na juisi hivyo
kupelekea vifo vya watoto hao.
Kamanda huyo alisema
,katika eneo la tukio kumeokotwa chupa mbili za juisi zilizotumika ,chupa ya
dawa na matapishi ambavyo vilichukuliwa kwa uchunguzi zaidi.
“Mara baada ya tukio
mtuhumiwa alikunywa sumu kwa lengo la kutaka kujiua lakini aliokolewa na watu
kisha kukimbizwa katika hospital ya mission Bwagala wilaya ya Mvomero kwa
matibabu” Wankyo aliweka bayana.
Mpaka sasa hali yake sio
nzuri kwani yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa chini ya uangalizi
wa polisi .
Katika hatua nyingine
,Wankyo alisema jeshi hilo
limekamata viroba saba vya bangi vilivyokuwa vikisafirishwa kwenye gari yenye
chesesi namba V75w – aina ya mitsubishi station wagon huko Kijiji cha Mwatemo kata ya Kiwangwa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment