Saturday, September 30, 2023

MUFTI ZUBEIR, AKAMILISHA ZIARA YAKE LEO NCHINI UINGEREZA.

 

Na Hamimu Mussa,
Afisa Habari Mkuu
Bakwata Online Academy
Ofisi Ya Mufti-Tanzania

Leo tatehe 30/09/2022, ndio siku ya mwisho ya ziara ya Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeir Bin Ally Nchini Uingereza ambapo ameweza kuitembelea miji mbalimbali na hasa yenye Waislaamu wengi Watanzania wanaoishi huko.


Jana tarehe 29/09/2023 akiwa katika Mji wa Leeds-Bangaladesh Center, aliweza kuwaaga diaspora wetu Nchini humo pamoja na wale wote walioshiriki katika Mkutano huo, ikiwa ni ishara ya ziara hiyo kufikia mwisho.


Inatajwa ni miongoni mwa ziara Bora kuwahi kufanywa na Viongozi wa kidini kutoka katika Mataifa ya kiafrika, na hii ni kwa sababu ya ujumbe aliokuwa nao kiongozi huyo Mkuu wa kidini Nchini Tanzania.


Ziara hiyo ilibeba ujumbe mzito kwa ulimwengu ikiwemo Amani kwa watu wote, uchumi, elimu, afya, chakula, teknolojia, usawa, haki na wajibu, maridhiano, mshikamano na umoja, uongozi na utawala bora pamoja utunzaji wa mazingira kwa kuvilinda viunbe hai.


Zaidi ya hapo, Mheshimiwa Mufti ameitumia ziara hiyo kwa kuwakumbusha Watanzania waishio katika Mataifa mengine (Diaspora) kuwekeza mitaji yao nyumbani ili iwe ni faida kwa Nchi na Watanzania kwa ujumla.





BAGAMOYO YATEKELEZA USAFI WA MWISHO WA MWEZI.

 

Viongozi mbalimbali katika Halmashauri ya Bagamoyo leo Tarehe 30 Septemba 2023 wameshiriki katika zoezi la usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wananchi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bagamoyo.


Akiongoza zoezi hilo la usafi wa mazingira ambalo hufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, kwaniaba ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda amesema usafi wa mazingira ni jambo la lazima kwa kila mwananchi ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.


Alisema swala la usafi wa mazingira sio hiyari kulitekeleza kwani mazingira safi humuacha mtu akiwa salama ki afya na muonekano.


Amewataka wananchi kufanya usafi wa mazingira kila siku, kila wiki na kujumuika pamoja kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.















MBUNGE PROF. MUHONGO NA WADAU WAFANIKISHA HARAMBEE UJENZI WA ETARO SEKENDARI KISIWA CHA RUKUBA

 


Na Mwandishi Wetu, Musoma Vijijini.


MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sosepter Muhongo kwa kushirikiana na viongozi wakiwemo wakuu wa Wilaya ya Musoma na Halmashauri yake (Musoma DC), waemeendesha Harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondati Etaro, ambayo itakuwa ya Kata hiyo katika kisiwa cha Rukuba.


Katika tukio hilo lililofanyika Septemba 27,2023 kwenye Kisiwa hicho,

Wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakiwemo Walimu, Kamati ya Siasa ya Wilaya na Wadau wengine wameshiriki


Kwa mujibu wa Ofisi ya Mbunge kupitia taarifa yake kwa umma, mapema leo Septemba 30,2023, imebainisha kuwa, Michango iliyopatikana kwenye Harambee hiyo ni pamoja na: 


"Wakazi na Wazaliwa wa Kisiwa cha Rukuba-Saruji Mifuko 167, Kamati ya Siasa ya Kata CCM-Saruji Mifuko 22, Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM-Saruji Mifuko 15 na DED na wenzake-Saruji Mifuko 20.


Wengine waliochangia kwenye Harambee hiyo ni: "DC na wenzake- Saruji Mifuko 62, Mbunge wa Jimbo hilo la Musoma Vijijini-Saruji Mifuko 200,


Aidha,Fedha taslimu,Tsh248,000 (zikiwemo Tsh 105,000 za Walimu Makada wa CCM).


"Karibuni tujenge Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba cha Musoma Vijijini.


Furaha na shauku ya ujenzi wa Sekondari Kisiwani Rukuba ni yetu sote" Imeeleza taarifa hiyo.


Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji vinne vya Kata ya Etaro ambapo Wanafunzi wa sekondari kutoka Kisiwani humo wanasoma nchi kavu kwenye sekondari ya Kata yao (Etaro Sekondari).


Ambapo imeelezwa kuwa, Wanafunzi hao wanakumbana na matatizo mengi ambayo yanadhoofisha maendeleo yao kielimu hivyo wakazi hao wameamua kujenga sekondari yao Kisiwani humo.


TOENI USHIRIKIANO KWA MIRADI YA TASAF- Ridhiwani Kikwete

 

Watumishi pamoja na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF)  ili kuwainua watu wenye uhitaji



Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaongea na wananchi wa kata ya Msata na Msoga katika mikutano baada ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).


Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya Msoga , na baadae kuona mafanikio ya miradi ya kuwezesha wananchi na miradi ya miundombinu ya jamii, 


Naibu Waziri aliwaomba wananchi na Halmashauri kuendelea kushirikiana na Miradi ya TASAF ili kuwanyanyua wananchi wenye uhitaji. 


Katika mkutano huo, Naibu Waziri aliwapongeza Halmashauri kwa kutenga pesa za kukopesha vikundi vya maendeleo vikiwemo vikundi vya wanufaika wa miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wameshukuru TASAF kwa jitihada za kuwakomboa katika hali mbaya ya umaskini na pia kuishukuru Halmashauri kwa kuendelea kutenga pesa kwa vikundi vikiwemo vya TASAF na mafanikio yanayoonekana ni kwa sababu ya mipango hii kufanywa pamoja. 

Halmashauri ya Chalinze imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali na katika mkutano huo pamoja na makundi mengine, vikundi viwili vya Pain For Success na Muungano ambavyo kila kimoja kilikopeshwa shilingi Milioni 10 vilitoa ushuhuda wa jinsi mipango hivyo ilivyofanikiwa kwa kuonyesha bidhaa mbalimbali walizotengeneza na miradi waliyoshiriki. 


MAGAZETI YA LEO TAREHE 30 SEPTEMBA 2023










WAZIRI MKUU AFUNGA MAFUNZO YA UHAMIAJI, AHIMIZA UADILIFU

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wahitimu 521 wa mafunzo ya Kozi Na. 01/2023 wakatumie vema ujuzi na maarifa waliyoyapata katika kudhibiti vitendo vya uhalifu hususan maeneo ya vipenyo, vituo na mipakani.

Ametoa wito huo leo Ijumaa (Septemba 29, 2023) alipofunga mafunzo hayo kwa askari wa Uhamiaji katika Chuo cha Mafunzo ya Uhamiaji cha Raphael Kubaga, Wilayani Mkinga, katika Mkoa wa Tanga.

Waziri Mkuu amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo mpango wake wa kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Mheshimiwa Majaliwa pia amewataka wahitimu hao wakafanye kazi kwa uzalendo, weledi na kutanguliza kwanza maslahi ya Taifa katika kazi zao za kila siku. “Kila mmoja akazingatie maadili na miiko ya kazi na akawe mfano bora wa uadilifu katika kituo atakachopangiwa,” amesisitiza.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa Jeshi la Uhamiaji wawachukulie hatua kali za kisheria wahitimu ambao watabainika kuwa wanajihusisha na vitendo viovu ikiwemo rushwa, wizi wa maduhuli ya Serikali, ama kujiunga na mitandao ya uhalifu wa kiuhamiaji.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kutokana na kuongezeka kwa teknolojia za kisasa na makosa ya kiuhalifu hususan biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu na uhamiaji haramu, wahitimu hao wanapaswa kuhakikisha wanapata maarifa mapya mara kwa mara ili waweze kukabiliana na mabadiliko hayo ya kiteknolojia.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa TARURA mkoa wa Tanga ahakikishe kuwa hadi kufikia mahafali ya mwaka 2024 awe ameijenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka barabara kuu inayoingia chuoni hapo.

Kuhusu changamoto ya maji kwa chuo pamoja na wananchi wa vijiji jirani, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Mamlaka za maji za Mkoa wa Tanga zihakikishe taasisi hiyo inaunganishwa kwenye mtandao wa maji. “Lakini pia Katibu Mkuu upo hapa, ona namna ya kuwezesha chuo hiki fedha kwa ajili ya ujenzi wa tanki la kuhifadhi kama yalivyo mahitaji ya chuo.”

Mapema, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni alisema awali Jeshi la Uhamiaji halikuwa likitoa mafunzo kwa watumishi wake.

"Mwaka jana ndiyo tulitoa kundi la kwanza la wahitimu, tunamshukuru Mhe Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa sh. bilioni 1.5 za kuendeleza majengo. Hatukuwa na ajira mpya katika idara ya uhamiaji, tunamshukuru kwa kuongeza ajira wakiwemo hawa 521 wanaohitimu leo," alisema.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mkinga, Bw. Dunstan Kitandula alisema anashukuru Serikali kwa uwepo wa chuo hicho na kuongeza: "Tunaiomba Serikali iendelee kuboresha chuo hiki kwa sababu matamanio yetu ni kuona chuo kinasaidia Afrika Mashariki yote."

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala aliiomba Serikali isaidie kuboresha miundombinu ya chuo hicho ikiwemo barabara ya kuingia chuoni na uwanja wa gwaride. Pia aliomba wajengewe tanki la lita 250,000 ili kutatua shida ya maji chuoni hapo na kwenye vijiji vya jirani.


Friday, September 29, 2023

TANZANIA KUSIMAMIA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI NA TAKA ZA KEMIKALI

 


Na. WAF - Bonn, Ujerumani

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya imesisitiza kuendelea kusimamia matumizi salama ya Kemikali na taka zitokanazo na Kemikali ili kuzuia athari kwa  wananchi.


Hayo yamebainishwa leo Septemba 29, 2023 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakati akiwasilisha tamko la Tanzania katika Mkutano wa tano wa Kimataifa wa Usimamizi wa matumizi salama ya Kemikali Duniani (ICCM5) kwa niaba ya Mhe Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.


Aidha, Dkt Magembe alieleza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuchukua hatua madhubuti kudhibiti matumizi mabaya ya Kemikali ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mazingira nchini kwa kutekeleza kwa vitendo malengo endelevu ya maendeleo ya Dunia na katika kujenga uchumi endelevu wa nchi.


“Pamoja na kuwa matumizi ya Kemikali  ni muhimu na zipo faida nyingi zitokanazo na kemikali hasa katika sekta za Afya, Kilimo, Elimu, Viwanda nk, shughuli za kemikali zisiposimamiwa vizuri, zinaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya binadamu,  mazingira, usalama mahala pa kazi, ulinzi na usalama wa nchi”. Amesema Dkt. Magembe.


Pia Dkt. Magembe amesema kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha, takribani vifo milioni mbili duniani  kwa mwaka vinatokana na matumizi mabaya ya Kemikali yakiwemo madhara mengine kama ulemavu, kuharibika kwa mimba, magonjwa ya mfumo wa hewa na saratani.


Sambamba na hilo Dkt. Magembe amebainisha mipango ya Tanzania katika matumizi ya kemikali hizo ikiwa ni Pamoja na kuimarisha uratibu na usimamizi wa Kemikali ndani ya nchi Pamoja na kutenga rasilimali za kutosha ikiwemo fedha ili kuwezesha utekelezaji wa mpango mkakati huo, hususani kuziwezesha nchi zinazoendelea kuzuia na kudhibiti madhara yatokanyo na matumizi ya Kemikali.


Aidha Dkt. Magembe ameziomba nchi zilizoendelea kushirikiana na nchi zinazoendelea katika kuwekeza kwenye teknolojia za kisasa kwenye viwanda vinavyozalisha dawa, vifaa tiba, mbolea, viuatilifu  na bidhaa nyinginezo kwa lengo la kuzalisha bidhaa rafiki kwa afya ya binadamu na mazingira na pia kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa hizo.

RAIS WA ZANZIBAR KATIKA SWALA YA IJUMAA,MASJID JAMIUU

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kulia) leo ameshiriki ibada ya swala ya ijumaa katika Masjid Jamiuu Zinjibar pamoja na Waumini wengine kama wanavyoonekana katika picha wakiitikia Dua iliyosomwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi  (katikati)  baada ya Ibada ya   Swala hiyo ya ijumaa, Mazizini  Mkoa wa Mjini Magharibi. [Picha na Ikulu] 29/09/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi pamoja na Viongozi wengine wakati alipowasili katika Masjid Jamiuu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi  leo kushiriki katika Swala ya Ijumaa. [Picha na Ikulu] 29/09/2023.

Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria Ibada ya Swala ya Ijumaa leo, Masjid Jamiuu Zinjibar,Mkoa wa Mjini Magharibi wakiitikia Dua Iliyoombwa baada ya  ibada hiyo, iliyowajumuisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na Viongozi mbali mbali. [Picha na Ikulu] 29/09/2023.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Sheikh Salum Mardhia baada ya kumalizika kwa ibada ya Sala ya Ijumaa Leo katika masjid Jamiuu Zinjibar Mazizini  Mkoa wa Mjini Magharibi. [Picha na Ikulu] 29/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiteta na Mkurugenzi wa Mkuu wa Kituo cha Ahmed Al Faatih  cha Kiislamu -Bahrain Bw.Nawaf Rasshid Al Rashid (katikati) baada ya Ibada ya   Swala ya Ijumaa katika  Masjid Jamiuu Zinjibar Mazizini  Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 29/09/2023.


TANZANIA YATANGAZA UTAJIRI WA MADINI MKAKATI UFARANSA

 

Dkt. Kiruswa asema Tanzania mdau muhimu kuokoa Dunia na uchafuzi wa mazingira.

Atumia jukwaa hilo kunadi fursa za uwekezaji nchini

......................

Paris, Ufaransa.

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye rasilimali madini kwa wingi yakiwemo Madini Mkakati ambayo mahitaji yake yanazidi kuongezeka kutokana na kutumika kuzalisha aina tofauti za vyanzo vya nishati na teknolojia zinazohitaji aina mbalimbali za madini mkakati kama vile Lithiamu, Nikeli, Kobalti, Manganese na Grafiti.


Ameyasema hayo Septemba 28, 2023, jijini Paris nchini Ufaransa wakati akihutubia Mkutano wa Kilele wa Usalama wa Madini Mkakati ambao umejadili masuala muhimu kuhusu madini hayo, kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili namna ya kushiriki katika kuchochea usimamizi na usambazaji endelevu wa madini hayo.


Alisema kuwa kutokana na mwelekeo wa sasa teknolojia, zinahitaji aina mbalimbali za madini mkakati na kwamba, nchini Tanzania madini hayo yanapatikana kwa wingi.


“Ndugu Washiriki, mengi ya madini mkakati yanayohitajika kwa mabadiliko ya nishati safi yanapatikana kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Hizi ni pamoja na rasilimali muhimu ya Grafiti, Nikeli, Kobalti, Lithiamu, Vipengee Adimu vya Dunia (Rare Earth Elements [REE]), Shaba, Manganese, Zinki na Alumini.” alisema Dkt. Kiruswa.


Aidha, Dkt. Kiruswa alisema kuwa kutokana na uwepo wa rasilimali hizo Tanzania ni miongoni mwa wadau muhimu katika Mkakati wa Mpito wa Nishati Safi kutokana na kuwa na Rasilimali Madini muhimu na Mkakati ya aina mbalimbali kwa kiasi kikubwa.


Sambamba na hilo, Dkt. Kiruswa aliueleza mkutano huo kuwa, miongoni mwa masuala yanayohitaji mkakati wa pamoja wa kimataifa, ni pamoja na namna bora ya ugavi wa madini hayo, uboreshaji wa uwazi wa masoko, kuongeza kasi ya teknolojia za uvumbuzi na uchakataji na kukuza mazoea ya maendeleo endelevu na yenye uwajibikaji.


Aidha, alitumia jukwaa hilo kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini na kuongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika ambazo zina amani na utulivu mkubwa kisiasa.


“Tanzania imeunganishwa vyema na mitandao mizuri ya barabara inayofanya mikoa na wilaya zote kufikika. Faida nyingine kubwa ya kuwekeza nchini Tanzania ni uwepo wa mfumo ujao wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) ambao unaendelea kujengwa kuanzia Bandari ya Dar es salaam hadi katika nchi jirani zisizo na bandari zikiwemo Rwanda, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)” aliongeza Dkt. Kiruswa.


Mbali na Naibu Waziri, wengine walioshiriki kutoka Wizara ya Madini ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Uendelezaji Migodi kutoka Wizara ya Madini, Terence Ngole, Kaimu Mkurugenzi wa Kanzidata kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) Hafsa Seif.


Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mawaziri, Wafanyabiashara, Wawekezaji, taasisi za kimataifa na taasisi za kiraia kutoka nchi tofauti Ulimwenguni.


Katika hatua nyingine Ujumbe huo wa Tanzania ulipata nafasi ya kuzungumza na wadau wengine wa Sekta ya Madini kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India ambapo ulizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kabir ambayo ni sehemu ya Shirika la Madini la Taifa Nchini India, lengo likiwa ni kuona namna nzuri ya kuanzisha ushirikiano wa kikazi na kubadilishana ujuzi kwenye Sekta ya Madini.





CP. WAKULYAMBA ATOA SOMO LA MIONGOZO YA JESHI LA UHIFADHI.

 

Na Sixmund Begashe


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba amewataka askari wa Jeshi la Uhifadhi kufanya kazi kwa kufuata Miongozo, Kanuni na kuzingatia sheria zilizopo ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Uhifadhi.

CP. Wakulyamba ametoa kauli hiyo Jijini Arusha kwenye Warsha maalum aliyoianda kwa Maafisa wa Jeshi la Uhifadhi chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kukumbushana masuala mbalimbali ya uhifadhi pamoja na haki za binadamu kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan la kumtaka arejeshe nidhamu ya Jeshi hilo.


Katika somo alilotoa kwa Maafisa hao wa Jeshi la Uhifadhi, CP. Wakulyamba alisisitiza nidhamu katika matumizi sahihi ya sare za Jeshi hilo pamoja na matumizi ya nguvu katika kukabiliana na uhalifu hususani kwenye matumizi ya Silaha.



Aidha CP. Wakulyamba amelitaka Jeshi hilo kuimarisha mahusiano mema na Vyombo vingine vya ulinzi na Usalama, taasisi za Serikali na wananchi kwa ujumla kuwa kazi ya uhifadhi ni jukumu la kila Mtanzania kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kinachokuja.












CHATANDA AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM WILAYANI CHATO. 

 


Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda, amefurahishwa na Utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani Chato Mkoani Geita alipotembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika wilaya hiyo .

Akizungumza leo  katika Mradi  wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato Mwenyekiti Chatanda amewapongeza viongozi wa Serikali chini ya Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedith Katwale ambaye ameshirikia na Mkurugenzi wake wa Halmashauri kwa usimamizi na Ufanisi wa hali ya Juu .

" Fedha ya Serikali zaidi ya Bilion 31 imejenga Hospitali hii ya Kanda ya Chato niwaombe wauguzi wa Hospitali hii muwahudumie wagonjwa vinzuri kwa kuwa wananchi mbalimbali watakuja kutibiwa hapa hivyo Uadilifu, upendo na hekima ili wananchi wafurahie matunda ya Rais Samia kwa upande wa  afya katika kupata huduma bora kwa wauguzi wao."