KLABU
ya Yanga imekubali kufanya uchaguzi, kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi,
Januari 13, mwakani huu.
Wiki mbili zilizopita Baraza la Michezo la Taifa (BMT), iliwataka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojiuzuru huku ikiwemo ya mwenyekiti wao wa zamani Yussuf Manji.
Yanga kwa sasa imebaki na wajumbe wanne kati ya wajumbe 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Thobias Lingalangala amesema kwamba wanatarajia kufanya uchaguzi mapema mwakani na fomu za kugombea tayari zimeshaanza kutolewa.
Lingalangala
amesema uchaguzi utafanyika kama ulivyotangazwa na kamati ya uchaguzi ya Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) na fomu zimeanza kutolewa rasmi leo ofisi za TFF na
klabuni.
Alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama walikuwa wanazuia uchaguzi huo ameomba wapuuzwe na wanachama wote w anaruhusiwa kuja kuchukua fomu kama anaona anafaa kuweza kuongoza klabu yao.
“Tumeanza kutoa fomu leo hivyo tunawaomba wanachama wenye nia ya kugombea waje kuchukua fomu na hata mwanachama pia kama unaona kuna mtu anafaa kugombea katika nafasi yeyote basi amshawishi ili aweze kuchukua fomu mapema,” alisema Lingalangala.
Hata hivyo Lingalangala alisisitiza kuwa kama itatokea wanachama au mwanachama yeyote ambaye atapinga uchaguzi huo basi watampeleka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili waweze kumpa adhabu inayostahili.
Hata hivyo Lingalangala alisema kuwa garama za fumu hizo nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni Sh. 200,000 na wajumbe wake ni sh.100,000.
Wakati huo huo kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga imemteua Lingalangala kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu hadi uchaguzi wa kujaza nafasi utakapofanyika.
Klabu ya Yanga imekuwa ikihairisha mara kwa mara kufanya uchaguzi wake, licha ya Juni 10 mwaka huu Waziri Mwakyembe kuwataka wafanye uchaguzi kuziba mapengo ambayo yapo wazi.
Kati ya viongozi wa klabu hiyo ambao waliingia madarakani Julai mwaka juzi, viongozi sita wamejiuzulu nafasi hizo wakidai kuwa na majukumu mengi.
Viongozi waliojiuzulu ndani ya klabu hiyo pamoja na Manji, wengine ni Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe Inspekta Hashim Abdallah, Salum Mkemi, Omary Said, Ayoub Nyenzi na huku waliobaki ni wajumbe Thobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Siza Lyimo na Hussein Nyika.
No comments:
Post a Comment