ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI NI NGAO YA TAIFA KATIKA VITA.
Ithibati ya waandishi wa habari imeendelea kujidhihirisha kama nguzo muhimu ya ulinzi wa Taifa katika dunia ya sasa inayotawaliwa na vita ya taarifa. Kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), inayotoa ithibati na vitambulisho vya uandishi wa habari kwa waandishi wenye vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, Taifa linapata waandishi wanaotambulika, wanaowajibika na wanaofanya kazi kwa kufuata misingi ya taaluma, weledi na maadili. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Greyson Msigwa, wakati akizungumza katika kikao kazi na waandishi wa habari kilichoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) tarehe 18 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa hatua hiyo inasaidia kudhibiti upotoshaji wa taarifa na kulinda taswira ya nchi ndani na nje ya mipaka yake kwani dunia ya sasa haipigani tena vita kwa silaha za kijeshi pekee, bali kwa taarifa zinazozalishwa ...