Posts

Showing posts from April, 2017

SERENGETI BOYS YAPONGEZWA KWA USHINDI.

Image
Serikali imeipongeza Serengeti Boys kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Gabon. Serengeti Boys wameifunga Gabon katika mechi iliyopigwa nchini Morocco ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika litakalofanyika nchini Gabon. Msemaji wa Serikali Dk, Hassan Abbas amesema serikali inaipongeza timu hiyo ya vijana chini ya miaka 17 kwa ushindi huo. Serikali inawasisitiza vijana hao kuendelea kupambana wakiwa wamelenga kufanya vizuri na Watanzania na serikali iko nyuma yao.

MAGAZETI YA LEO 16 APRILI 2017.

Image

YANGA YATOA KAULI POITI 3 ZA SIMBA.

Image
Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi tatu. Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na mabao matatu ikiwa ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna wanachama wanataka kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku akisisitiza Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka Kombe la Dunia itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”. “Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la Dunia tena. ”Watu wana hasira zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea. Kagera ni timu ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii kesi. “Ajabu kabisa, waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si sawa, kuna jambo hapa,” alihoji Mkemi akione...

MAUJAJI YA POLISI, RAIS DKT. MAGUFULI ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.

Image
 

MAJAMBAZI YAUA POLISI NANE PWANI.

Image
Askari polisi   nane wameuwawa na Majambazi mkoani   Pwani. Tukio hilo   limetokea majira ya   saa 12 na robo jioni   ya   Tarehe 13 Aprili 2017 huko eneo   la Mkengeni kijiji cha   Uchembe kata ya Mjawa Tarafa   ya Kibiti Wilayani Kibiti   Mkoa wa   Pwani. Ambapo kundi   la majambazi   ambalo idadi yake bado   haijafahamika wakiwa na silaha   walishammbulia kwa risasi Gari la   Polisi lenye namba za usajili PT. 3713   TOYOTA Land Cruiser na kuuwa Askari nane na mwingine mmoja kujeruhiwa mkononi. Aidha, baada ya   majambazi hao kufanya mauaji walifanikiwa   pia   kuchukua silahatisa kati ya hizo SMG sita zikiwa na risasi 30, kila moja na   Long Range   tatu. Awali Gari ya   Polisi ilikuwa   ikitokea jarikbu   mpakani kwenye   kizuizi kuelekea Bungu baada ya   kubadilishana zamu ambapo walipofika eneo la Mkengeni   sehemu yenye m...

KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINT TATU.

Image
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 imeipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu kutokana na rufaa waliyoikatia Kagera Sugar kwa kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 2, mwaka huu. Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba badala ya mchezaji huyo kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizopata mfululizo. Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku wa April 13, 2017 kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi. Kwa ushindi huo, Simba sasa inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 26, wakiendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania bara mbele ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 56 wakiwa wamecheza mechi 25. Ikumbukwe Simba iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe...