MWONGOZO WA KUWARUDISHA SHULE WALIOPATA MIMBA WAANDALIWA.
Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu kutoka shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI) mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen akitoa neno fupi kwa ajili ya kuwakaribisha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu. Ufunguzi wa warsha hiyo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali wanaohusika na elimu kutoka nchi sita za ...