Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya kazi za wanafunzi wakati
wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Mihadhara na Bweni la Wanafunzi katika chuo
cha Misitu, Olmotonyi, Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
.................................................................
Na Amiri Mvungi-Arusha
Makamu
wa rais mheshimiwa Samia Uuluhu Hassan ameeleza kutokuridhishwa na
utekelezaji wa agizo la ofisi yake kwa halmashauri za wilaya kote nchini
kupanda miti akibainisha kuwepo kwa udanganyifu wa takwimu zinazotolewa za
idadi ya miti inayopandwa.
Akizungumza
mara baada ya kuzindua rasmi majengo ya mabweni na ukumbi wa mihadhara
yaliyojengwa katika chuo cha mafunzo ya misitu olmotonyi,mama Samia Suluhu amesema
bado hali ya mazingira nchini sio ya kuridhisha na hapa anaagiza kuwa ni
vyema miti inayopamdwa ijumuishwe na miti ya mazao…mh samia suluhu-makamu
wa rais.
Ujenzi
wa majengo hayo yaliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja nukta
nane ni moja ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji shirikishi wa misitu
unaofadhiliwa na serikali ya norway majengo ambayo naibu waziri wa maliasilina
utalii Japhet Hasunga anasema licha ya kuwapunguzia adha wanafunzi wa kike
waliokuwa wakiishi nje ya chuo pia yataongeza kasi ya udahili…japhet hasunga
..naibu waziri maliasili na utalii.
Elisabeth
Jacobsen ndiye balozi wa norway hapa nchini ,anasema ufadhili huo
unalenga kudumisha ushirikiano na tanzania katika kukabiliana na athari
za mabadiliko ya tabia nchi yanayoonekana kuathiri mataifa yote
ulimwenguni..elisabeth jacobsen-balozi wa norway nchini.
No comments:
Post a Comment