Mbunge wa viti maalu
kupitia CCM kutokea mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu akizungumza na wazazi wa mkoa
huo.
Na Shushu
Joel,Mlandizi.
MBUNGE wa
viti maalumu mkoa wa Pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM Zaynabu Vulu
amewataka wazazi na walezi wote mkoani humo kutambua kuwa uamuzi wa
serikali katika kutoa elimu bure haitomuomdolea mzazi au mlezi wajibu wake wa
kumtuza mtoto kwa ajili ya mahitaji yake pindi anapokuwa shuleni ambayo ni
nguo,madaftari na mchango wa chakula ili kuimalisha afya ya mwanafunzi katika
uelewa wake masomoni.
Elimu ni
nguzo kubwa kwa mahitaji ya wataalamu katika nchi yeyote ile kwa lengo la kuendesha
shughuli za serikali hivyo wazazi na walezi kwa pamoja wanamajukumu ya kuwajali
kwa kuwatimizia mahitaji yao ya kila siku watoto wao.
Kauli hiyo
aliitoa jana alipokuwa katika mkutano na mwenyekiti wa UWT uliokuwa ukiwahamasisha
wazazi kutambua wajibu wao kwa watoto wao na si kila jambo la shule waliachie
serikali.
Aliongeza
kuwa madhumuni ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bure kuanzia darasa la kwanza
mpaka kidato cha nne kwa lengo la kuwapunguzia wazazi mzigo mzito na pia
ilikuwa ni moja ya sera ya CCM katika kujinadi walipokuwa wakiomba ridhaa kwa
wananchi pindi walipokuwa wakiomba nafasi ya kuwatumikia.
“Serikali ya
awamu ya ano imeamua kuwekeza katika elimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa,na
kwamba kwa kutoa fursa hiyo kumetengeneza idadi kubwa ya watoto walioandikishwa
kuanza darsa la kwanza mwaka huu na wale wanaoingia kidato cha kwanza nchini
kote”Alisema Vulu.
Aliongeza
kuwa baadhi ya wazazi wanapaswa kubadilika kwani wamekuwa wakibweteka na mpango
wa serikali ya awamu ya tano katika utoaji wa elimu bure,wamekuwa hawataki
kujishughulisha hata kwa uhitaji wa manunuzi ya mahitaji muhimu ya wanafunzi
shuleni.
Katika
taarifa yake katibu wa UWT mkoa wa Pwani Mwajuma Nyamka alisema kuwa tangu
kutangazwa kwa elimu bure kumekuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wazazi
wakidai ni kwanini watoto wasinunuliwe nguo za shule pia ilivyo kwa ada,kitu
ambacho amekuwa akikitolea ufafafuzi mkubwa kwa wazazi na walezi walio wengi
kutambua umuhimu na nafasi zao katika familia zao.
Alisema kuwa
katika suala la serikali serikali kuwasaidia wazazi katika jambo la ada basi
wazazi na walezi wengi wamekuwa wakihitaji kila kitu serikali ifanye kupitia
wanafunzi wao walioko mashuleni kitu ambacho si sahihi kutokana na kuwa
serikali inahitajika kufanikisha maendeleo katika kila nyanja ili wananchi wote
waweze kupata huduma za kijamii kwa wakati.
Naye
mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Farida Mgomi amempongeza mbunge huyo kwa kutoa
neno lilikuwa likiwaumiza kichwa wao kama viongozi wa kisiasa kwa wananchi
wao,hivyo amewataka viongozi wote wanapokuwa na shughuli za kukutana na
wananchi wanapaswa kulisema hilo kwa baadhi ya wananchi wasiotaka kubadilika
kwa watoto wao ambao wanakosa hata nafasi ya kupumua kwa hofu ya kulipa ada.
Aidha
amewapongeza wazazi wote waliojitokeza katika mkutano huo na
kuwahakikishia shuwa serikali itaendeleo kuwasaidia wananchi wote katika
kuhakikisha elimu bure inakwenda mbali zaidi ya hapo ilipo sasa.
Hivyo Mgomi
alitumia fursa hiyo kuwataka kinamama wote mkoa wa Pwani kuhakikisha
wanachangamkia fursa za mikopozilizoko katika halmashauri za mkoa huo ili
kujikwamua katika uchumi wa viwanda ambapo mkoa huo umezidi kujichukulia
umaarufu wa kuongoza katika sekta hiyo.
Zaynabu Vulu akimsikiliza
moja wa wazazi hayupo pichani juu ya sula la elimu bure .
No comments:
Post a Comment