Posts

Showing posts from November, 2025

TBN YAFAFANUA MKUTANO NA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU.

Image
  Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) Unatoa Ufafanuzi Kuhusu Mkutano wa Ikulu Dar es Salaam. Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) unapenda kutoa ufafanuzi rasmi na kuweka mambo wazi kufuatia taarifa zisizo sahihi na zinazoleta utata zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano uliofanyika hivi karibuni Ikulu. TBN inakanusha vikali madai yanayosambazwa na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, wakidai—bila uthibitisho wowote—kuwa wanahabari wa maudhui ya mtandaoni waliitwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la "kupewa maelekezo" kuhusu maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika tarehe 9 Desemba. Kusudi Halisi la Mkutano TBN inathibitisha kuwa madai haya si sahihi na yamekuwa yakipotoshwa. Kusudi la kweli na la moja kwa moja la wito wa Ikulu lilikuwa hili: Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Bakari Machumu, alifanya mkutano wa utambulisho rasmi na wadau muhimu wa sekta ya habari, akianza na wanahabari wa maudhui ya mtandaoni. Mkutano huu ulikuwa ni hatua muh...

MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU AKUTANA NA MTANDAO WA WANABLOGU TANZANIA (TBN) NA WAANDISHI WA HABATI ZA MTANDAONI.

Image
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kupokea maoni yao, ikiwa ni mfululizo wa mikutano na wadau wa Tasnia ya Habari kwa ajili ya kuboresha masuala mbalimbali ya Mawasiliano baina ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na Vyombo vya Habari, tarehe 27 Novemba, 2025. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba, 2025. Viongozi mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja cha Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, Wanablogu mbalimbali pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025. Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali wakizungumza katika Kik...