BAGAMOYO YAZINDUA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akiandaa sindano kwaajili ya uzinduzi wa chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akizungumza kabla ya kuzindua chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14. ....................................... Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga amesema mtu atakaekwamisha zoezi la chanjo ya Saratani ya shingo ya Kizazi atachukuliwa hatua za kisheria. Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze wakati wa uzinduzi wa chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi. Alisema serikali inapanga mikakti ya kuboresha Afya za wananchi wake ili waweze kutumikia taifa pamoja na kuihudumia wenyewe na familia zao. Aliongeza kuwa, Bagamoyo ina mikakati ya kukuza uchumi kwa kujenga viwanda hivyo ni wazi kuwa wanaotakiwa kufanya kazi katika viwanda hivyo ni watu wenye afya nzuri...