Posts

Showing posts from August, 2016

HALMASHAURI YA BAGAMOYO, YAFANIKIWA KUKUSANYA MAPATO MARA KUMI ZAIDI.

Image
Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy, kushoto, na kulia ni Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamedi Usinga ................................. Ukusanyaji mapato ya ndani katika Halmashauri ya   Bagamoyo umeongezeka mara   kumi   zaidi ukilinganisha na siku   za nyuma. Hayo yamebaishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Halmashauri mara baada ya kumaliza kikao cha baraza la madiwani kilichomalizika   leo. Mwenyeki huyo wa Halmashauri alisema kuwa Halmashauri ya Bagamoyo imejipanga vizuri katika vyanzo vyake vya mapato ili kukusanya mapoto halisi yanayo   kusudiwa na kufikia lengo lililowekwa na Halmashauri katika   kukusanya   mapato ya   ndani. Aliongeza kuwa utekelezaji   wa miradi   mbalimbali ya   maendeleo unategemea ukusanyaji mzuri wa mapato ambapo kwa namna walivyojipanga wameweza kukusany...

SERIKALI YA TANZANIA YAENDELEA KUPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA.

Image
Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati wa ufungaji wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo.   Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakimsikiliza Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu wakati wa ufungaji wa kikao kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam. ....................................... Serikali ya ...

DOTO M. JAMES, ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO.

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Doto M.James aliyeteuliwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.