Na
Shushu Joel,Chalinze.
MFANYABIASHARA
mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam Innocent Kimaro ambaye anajihusisha na
uuzaji wa madini ya mawe aina ya Dolomite ambayo hutumika viwandani kwa
ajili ya kutengenezea Vigae katika wilaya ya Bagamoyo Halmashauri ya chalinze
mkoani Pwani anatuhumiwa kutumia jina la mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete
kwa ajili ya kukwepa kulipa kodi na kupitisha mizigo yake bure kwa kuwatishia
wahusika wa kulipisha ushuru.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwenyekiti wa kijiji cha msoga Ramadhani Mrisho ambapo
mawe hayo yanachimbwa alisema kuwa mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa
jina la Innocenty Kimaro amekuwa akikataa kulipa kodi pindi anapopitisha mizigo
yake kwenye mageti kwa kudai kuwa yeye ni mtu wa karibu na mbunge wa
jimbo hilo (Ridhiwani Kikwete) hivyo si sahihi yeye kulipa kodi kwenye eneo
hilo.
Aliongeza
kuwa magari yake yanaposimamishwa kwenye mageti ili aweze kulipa ushuru
madereva wake wamekuwa wakikaidi kusimama kwa ajili ya ukaguzi wa malipo ya
halmashauri ya chalinze na hivyo kusababisha hasara kubwa kutokana na kutolipa
ushuru huo.
Aliongeza
kuwa kutokana na hali hiyo ya magari hayo kushamili kwa kupita kwenye sehemu za
kulipia ushuru bila kulipa niliwashauri wale vijana wanaokatisha ushuru waende
wakaombe msaada kwa matrafiki ili gari hizo ziweze kusimamishwa kwa lengo la
kujua kama kwamba wanalipa ushuru kijiji cha msolwa ambako ndiko mawe hayo
yanachimbwa na mfanyabiashara huyo.
“Mara baada
ya kuomba msaada wa matrafiki kuzisimamisha gari hizo na kisha madereva
kuulizwa ni kwanini awasimami getini walimpigia simu boss wao ambaye ni
Innocent Kimaro na kufika kwenye eneo la tukio na kuweza kulipa ushuru huo huku
akiwaambia hata mizigo ya Kikwete nayo inalipishwa ushuru”
Aidha
mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa akitumia jina
la Ridhiwani Kikwete kwa madai ya kuwa hata mbunge wenu mnamtoza kodi huku
wawekezaji amewaleta yeye kitu ambacho kinatufanya kujiuliza maswali mengi juu
ya jambo hilo,kwani mbunge hajawai kuwa na biashara na asilipe kodi.
“Mara
kwa mara tumekuwa tukiyasimamisha magari yake kwenye ili aweze kulipa ushuru wa
maeneo ambayo anachimba madini hayo lakini mtu huyo amekuwa akikaidi na magari
yake kuendelea na safari zake” Alisema Mrisho Mwenyeki wa kijiji cha msoga.
Mwandishi
wa habari hizi alimtafuta mfanyabiashara huyo ili kujibu tuhuma hizo ambae
alizungumza kwa njia ya simu na kusema kuwa yeye analipa kila kitu na wala hajawai
kutumia jina la mtu ili kukwepa kodi.
Akizunguza
juu ya kutumiwa kwa jina lake mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa
amesononeshwa na taarifa hizo kwa baadhi ya watu kutumia jina lake kwa ajili ya
kuibia mapato serikali na hivyo ameshauri mtu huyo atafutwe ili aweze kupigiwa
hesabu ili aweze kulipa madeni yote anayodaiwa.
Aliongeza
kuwa simjui wala sina biashara ya mawe na hata kama ningekuwa nayo ni lazima
hata mimi ningelipa ushuru ili kuliongezea pato taofa langu.
Aidha
mbunge huyo alisema kuwa mpaka kipindi hiki anafanya mazungumza na wamiliki wa
kiwanda ambacho mkwepa ushuru huyo anapeleka madini hayo kwa lengo la kujua
amepeleka mara ngapi ili gari hizo zipigiwe hesabu yake kwa lengo la kulipa
kodi za nyuma ambazo alipitisha bila kulipa ushuru wa halmashauri.
Kutokana
na hali hiyo Ridhiwani Kikwete amesema kuwa hatawafumbia macho wale wote wenye
lengo la kutaka kumchafulia taswira yake aliyonayo katika jamii.
No comments:
Post a Comment