Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni
ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
“Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
...............................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
ametoa maagizo kwa kila Mkuu wa Mkoa aifanye afya ya uzazi na mtoto kuwa ajenda
ya kudumu katika vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC).
Makamu
wa Rais ametoa maagizo hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Jiongeze
Tuwavushe Salama” ya Kuongeza kasi ya Uwajibikaji Kupunguza Vifo Vitokanavyo na
Uzazi na Watoto Wachanga.
“Ili
kuhakikisha suala la kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto katika
nchi yetu linapewa kipaumbele cha juu katika shughuli za Serikali za kila siku”
alisema Makamu wa Rais
Tafiti
zilizofanyika mwaka 2015/2016 zinaonyesha kuwa, kiwango cha vifo vitokanavyo na
uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila
mwaka ambayo ni sawa na wanawake 30 hufariki kila siku, kutokana na matatizo
yatokanayo na uzazi na kwa uapnde wa watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai
1000 .
Makamu
wa Rais amesema jamii ina jukumu zito la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na
watoto wachanga kwa kuhakikisha kuwa inajiwekea mpango mahsusi wa rufaa wakati
wa dharura na utambuzi wa dalili hatarishi kwa mama na mtoto mchanga.
“Nitoe
rai kwa wananchi, wanawake na wanaume na vijana kujitokeza kuchangia damu mara
kwa mara kwa kuwa wakifanya hivi wanaokoa maisha ya mama mjamzito na watoto.”
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya damu salama inatumika kwa wakina mama
wajawazito na watoto alisema Makamu wa Rais.
Kauli
mbiu ya kampeni hii “Jiongeze: Tuwavushe Salama” inaaminika inaaminika italeta
matokeo chanya katika kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga
nchini.
Kwa
Upande mwingine Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kuwa mlezi wa
kampeni hiyo ambayo itatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, pia alimshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa
kipaumbele kwa afya ya Mtanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha taarifa inavyoonyesha hali halisi
ilivyo sasa katika masuala yanayohusu uzazi salama wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya
“Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazeena Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
“Jiongeze Tuwavushe Salama” ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo
ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Sehemu ya Wageni kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi
vitendea kazi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Binilith Mahenge (kushoto) mara
baada ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais.
No comments:
Post a Comment