Mkuu
wa Wilaya ya Arumeru *Mhe. Jery Muro* amejitolea kuwasadia kuandika
Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara
ili waweze *KUKOPESHEKA* na taasisi za Kifedha ambazo kabla ya kutoa msaada au
mkopo huitaji mchanganuo au Andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha
wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.
Mhe
Muro amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo Kwa *VIKWAZO* vya maandiko ya
Mradi katika hatua za awali Pinda *wananchi* wenye nia ya kuanzisha kilimo na
ufugaji wa kibiashara wanapoanza safari ya kutimiza *ndoto* zao za kuwekeza
katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa *vikwazo* hivyo aliamua
kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia
*wananchi* kuondoa Vikwazo hivyo.
Mhe
Muro amesema *tayari* kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima *( PASS)*
Private Agricultural Sector Support imekubalKuwaandalia na kugharamikia Mpango
Kazi wa kibiashara *( Bussiness Planning )* zitakazowasaidia Wakulima na
Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia
katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara.
Hatua
hiyo imefikiwa mara baada ya Mhe Muro kufunga *MAONYESHO YA JUKWAA LA WAKULIMA
MERU* ambayo yamefanyika Kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na
wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo pamoja na kukubali
kutoa msaada wa BURE katika kuandaa na kuandika maandiko ya mchanganuo wa
kibiashara pia amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za
kilimo na ufugaji *JUKWAA LA WAKULIMA MERU* ili kuwawezesha kufanya kazi zao
Kwa Haraka zaidi, na kuhaidi kuwatafutia Computer Kwa ajili ya kuhifadhi
kumbukumbu Za taarifa za wakulima na wafugaji.
Kwa
upande Meneja wa Tawi la kampuni ya *( PASS)* amempongeza Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru MHE Jerry Muro Kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo
amewataka wananchi hao Kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na
Taasisi hiyo.
*Imetolewa
na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru*
No comments:
Post a Comment