Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza
tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye RAHEL MATALAKA, miaka 41, mkazi wa kijiji
cha lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye
MALIATABU CONSTANTINE, miaka 10, mwanafunza wa darasa la pili shule ya msingi
Ikelege.
Tukio hilo la mauaji limetokea tarehe
03.11.2018 majira ya 19:00hrs usiku, hii ni baada ya mama wa marehemu kuletewa
malalamiko kuwa mtoto wake alikua akiangusha na kuiba maembe kwa jirani. Ndipo
mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu
mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea mtoto kupoteza fahamu na baadae
kufariki dunia.
Mtuhumiwa alipoona mtoto amepoteza
maisha alimchukua na kumtundika juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha khanga
ili apoteze ushahidi ili baadae ionekane kuwa amejinyonga. Ndipo majirani
walipoona tukio hilo walitoa taarifa kituo cha Polisi. Aidha baada ya
polisi kupata taarifa hizo tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio
na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Polisi tunaendelea na mahojiano na
mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Mwili
wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa ajili ya mazishi.
Katika tukio la pili, Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kukamata gari moja lililoibiwa lenye namba T.233
CDG aina ya Toyota Carina mali ya RENATUS ELIUS, mkazi wa mtaa wa Ghana, likiwa
limetelekezwa kando ya barabara huko maeneo ya Kitangiri Wilayani Ilemela.
Gari hilo liliibiwa tarehe
01.11.2018, ndipo mmiliki wa gari alitoa taarifa polisi juu ya kuibiwa kwa gari
lake. Polisi baada ya kupata taarifa hizo tulifanya msako mkali kwa
kushirikisha vikosi vyetu vya askari wa kufuatilia wezi wa magari na
Intelejensia. Ndipo tarehe 04.11.2018 majira ya mchana tulifanikiwa kulikamata
gari hilo likiwa limetelekezwa kando ya barabara huko mtaa wa kitangiri huku
wezi wakiwa wametoroka.
Aidha baada ya kulikamata gari hilo,
tulilifanyia ukaguzi na kugundua baadhi ya vifaa vya gari hilo vimetolewa
ambavyo ni betrii ya gari moja, tairi ya gari moja, jeki moja, radio ya
gari, power window na show ya mbele ya gari. Polisi tunaendelea na msako mkali
wa kuhakikisha wezi hao wanapatikana.
Katika tukio la tatu, Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye MALAGALITA MATHIAS, miaka
55, mkazi wa kijiji cha Nyatukala, kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi
(gongo) kiasi cha lita 20 na dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilo
moja, huko maene ya kijiji cha Nyatukala Wilayani Sengerema.
Tukio hilo limetokea tarehe
05/11/2018 majira ya 17:00hrs jioni, hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa
kwamba katika Vijiji vya Nyamizeze na Nyatukala vilivyopo Wilayani Sengerema
wapo watu wanaojihusisha na uuzaji pamoja na utengenezaji wa pombe ya gongo na
dawa za kulevya aina ya mirungi.
Aidha baada ya kupatikana kwa taarifa
hizo Polisi tulifanya msako mkali katika vijiji hivyo na kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi na mirungi huku
wenzake wakifanikiwa kutoroka.
Polisi tunaendelea na mahojiano na
mtuhumiwa ili kuweza kubaini wenzake anaoshirikiana nao katika biashara hiyo
haramu ya gongo na mirungu, pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani.
Katika tukio la nne, mtoto mmoja wa
kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 2 hadi 3 ameokotwa akiwa hai baada ya
kutupwa kichakani kandokando mwa ziwa Victoria na mtu asiyefahamika, huko
maeneo ya Bwiru ziwani Wilayani Ilemela.
Tukio hilo limetokea tarehe
01.11.2018 majira ya 14:00hrs, hii ni baada ya watu waliokua wakipita njiani
kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani ndipo walifuatilia na walipoona ni
mtoto walitoa taatifa polisi.
Polisi tulifanya ufuatiliaji wa
haraka hadi eneo la tukio na kukuta mtoto wa kike akiwa ametupwa kichakani hapo
akiwa hai huku mwiliwake ukiwa umeviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.
Mtoto amepata matibabu na hali yake
inaendelea vizuri amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru
Wilayani Ilemela kwa ajili ya hifadhi. Polisi tunaendelea na upelelezi
pamoja na msako mkali wa kumtafuta mama wa mtoto huyo.
Katika tukio la tano; Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mwanza tunamshikilia tapeli/mwizi mmoja aliyefahamika kwa jina la BENEDICTO
BAHATI, miaka 29, mkazi wa kiloleli, kwa tuhuma za kujifanya afisa wa TCRA,
kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Tukio hilo limetokea tarehe
02.11.2018, majira ya 16:30hrs, hii ni baada ya mtuhumiwa kwenda kwa mtumishi
wa benki ya CRDB tawi la Nyegezi -Malimbe na kumtapeli kuwa yeye ni afisa wa
TCRA Mkoa wa Mwanza, hivyo amefika hapo akidai anazo taarifa zake ambazo
zinaonesha amekuwa akifanya mawasiliano yasiyo rasmi.
Hivyo ametumwa na ofisi ya TCRA
Mwanza kufuatilia taarifa hizo, na kumtaka atoe fedha kiasi cha laki tano ili
aweze kumfichia siri ili asitoe taarifa hizo kwa mamlaka inayohusika yaani
TCRA.
Baada ya hapo mlalamikaji alitoa
taarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo Polisi tulituma askari makachero na wamakosa
ya mtandao na badae tulifanikiwa kumtia tapeli huyo nguvuni.
Polisi tunaendelea
na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika Mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani.Aidha msako mkali wa kuwatafuta wenzeka anaoshirikiana nao katika
uhalifu huo bado unaendelea.
Tukio la sita, Mafanikio ya misako
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kukamata gari moja aina ya IST
rangi ya Silver lenye namba T.892 DFY/DKY na pikipiki mbili moja inanamba
MC.836 ASK aina ya BOXER na nyingine aina ya FEKON lakini haina namba. Gari na
pikipiki hizo zimekamatwa baada ya kutumika katika matukio ya kiuhalifu katika
maeneo mbalimbali ya Jiji na Mkoa wa Mwanza.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,
tunatoa onyo kwa wakazi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza tukiwataka waache vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto, pindi mtoto anapokosea apewe kalipio na akanywe
na kuonyeshwa madhara ya wizi ili atambue kosa na wala sio vipigo.
Sambamba na
hilo tunawataka vijana waache tabia ya kujihusisha na uhalifu kwani
utawagharimu.
No comments:
Post a Comment