Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh. Julius
Kalanga Laizer mbunge wa jimbo la Monduli leo Bungeni jijini Dodoma.
..................................................
Spika wa Bunge la Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo amewaapisha wabunge wanne ambao walishinda
katika chaguzi ndogo zilizofanyika katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe,Monduli na
Liwale.
Mara Baada ya kufungua kikao cha 13
cha Bunge la 11 Spika Ndugai alianza kwa kumwita Mh Julius Kalanga Laizer wa
Monduli,Mh Mwita Mwikwabe Waitara Mbunge wa Ukonga,Mh Timotheo Paul Mnzava
Mbunge wa Korogwe Vijijini na Mh Zuberi Mohamed Kuchauka amabao wote ni
kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Mara baada ya kumaliza kuwaapisha
wabunge hao spika aliendelea na shughuli za bunge kama zilivyopangwa ambapo
mapendekezo ya mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na
serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 .
Pia aliomba alimtaka Mwenyekiti wa
kamati ya bajeti kutoa taharifa kuhusu mapendekezo ya mipango wa Maendleo wa
Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango
wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mh Spika pia alimwita Msemaji Mkuu wa
kambi ya upinzani wa Wizara ya fedha na Mipango kuhusu mapendekezo ya mpango wa
Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na mwongozo wa
kuandaa mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2019/2020.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mwita Mwikwabe Waitara mbunge wa jimbo la
Ukonga leo Bungeni jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh Timotheo Paul Mnzava mbunge wa
jimbo la Korogwe Vijijini leo Bungeni jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh Zuberi Mohamed Kuchauka mbunge wa jimbo
la Liwale leo Bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Monduli Mh. Julius Laizer
Kalanga akipongezwa na baadhi ya wananchi waliofika bungeni kumpongeza.
Mh Zuberi Mohamed Kuchauka mbunge wa jimbo la
Liwale kushoto akiwa na wananchi kutoka Liwale waliofika kumpongeza.
Mh Timotheo Paul Mnzava mbunge wa jimbo la
Korogwe Vijijini akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa
bungeni jijini Dodoma leo.
Mh. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Mh. Mwita Mwikwabe Waitara pamoja na familia yake.
PICHA NA JOHN BUKUKU-BUNGENI JIJINI DODOMA
No comments:
Post a Comment