Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) mkoani Pwani, umempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kasi yake ya utekelezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo miradi ya REA awamu ya III kwa vijiji 150 na mradi mkubwa wa Rufiji Hydropower utakaozalisha 2,100 MW baada ya kukamilika.
Aidha
wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga bajeti ya bilioni 12.4 kwa
ujenzi wa vituo 18 vya afya mkoa mzima na hospital tatu Kibaha Mjini, Kibaha
Vijijini na Kibiti.
Mbunge
wa viti maalum Mkoa wa Pwani, ambae pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Hamisi Mgalu alisema anampongeza Rais Dkt. Magufuli kutokana na uongozi wake kwa
kutekeleza ahadi mbalimbali kwa wananchi.
Alisema wakati anaingia madarakani Mh. Rais
Magufuli alikuta asilimia 38 ya wanaopata huduma za umeme lakini sasa ni
asilimia 60 wamepata umeme kupitia miradi iliyokaribu nao, na miradi ya umeme
vijijini.
Subira
alielezea, kuna REA awamu ya tatu ambayo inaendelea ambapo vijiji 7,873
vilikuwa havina umeme lakini kwa kazi inayoendelea mzunguko wa kwanza vijiji
3,559 vinafanyiwa kazi na wakandarasi wapo kazini.
Alibainisha
kwamba, kulikuwa na mradi wa ujazilizi ambapo vijiji 105 vimepata umeme na
wananchi zaidi ya 25,000 kwenye mikoa nane ukiwemo Pwani wameunganishiwa umeme
na mradi unaendelea.
Hata
hivyo alisema, serikali hiyo imeweza kufanikisha miradi ya maji katika miji ya
Bagamoyo, Kibiti ,Utete pamoja na mradi wa maji WAMI -Chalinze ,Ruvu -Chalinze
-Msoga, mradi wa maji katika miji ya Kisarawe na Mkuranga.
Subira
alitaja ujenzi wa barabara kwa makao makuu ya wilaya ya Kibaha, Kisarawe,
Mkuranga na Bagamoyo na upatikanaji wa dawa za kutosha kwenye vituo vya afya,
zahanati na hospital za wilaya.
Nae
mwenyekiti wa UWT Pwani, Farida Mgomi aliishukuru serikali kwa utoaji elimu
bure kwa shule za msingi na sekondari .
Ukarabati
wa miundombinu ya elimu kwa shule kongwe za sekondari Kibiti, Kibaha, Ruvu,
Minaki ,Kikaro, Mtanga Delta, Nyamisati na shule za msingi maeneo mbalimbali
mkoani hapo.
Mgomi
alitaja mafanikio mengine ,kuwa ni ununuzi wa boti kwa ajili ya visiwa vya
wilaya za Rufiji ,Kibiti na Mafia milioni 600.
“Ujenzi
wa gati la Nyamisati -Mafia bilioni14 ,miradi ya REA III kwa vijiji 150.
Wajumbe
hao kwa umoja wao walipongeza mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta mbalimbali
kwa kipindi alichokuwepo madarakani Rais. Dk Magufuli. “alisema Farida.
Wajumbe
wote kwa umoja wao walipongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali kutatua
kero mbalimbali kwenye sekta ya afya, nishati, maji, elimu na huduma za kijamii
.
Walimtakia
afya njema Rais,makamu wa Rais Samia Suluhu na waziri mkuu Kassim
Majaliwa.
Mkutano
huo wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) umefanyika katika kusherehekea
na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa
kutimiza miaka mitatu akiwa madarakani huku kukiwa na mafanikio katika jamii
Mwenyekiti wa UWT Pwani, Farida Mgomi akizungumza katika sherehe hiyo.
Mwenyekiti
wa UWT wilaya ya Bagamoyo, Rukia Masenga akizungumza katika shrehe hiyo.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu akizungumza katika sherehe hiyo.
Mwenyekiti wa UWT Pwani, Farida Mgomi akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa viti maalu mkoa wa Pwani, Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Bagamoyo, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Bagamoyo Rukia Masenga pamoja na viongozi waandamizi wa UWT Pwani.
Picha
ya pamoja viongozi wa UWT Pwani na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment