Anaandika
Mh.Jumaa Hamidu Aweso.
..
..
“Ndugu
zangu Nina furaha sana huenda zaidi ya siku zote ukitoa siku niliopata ridhaa
ya kuaminiwa na wana Pangani kua Mbunge wao.Asanteni sana.!
..
Kitu
kinachoifanya siku hii ya leo kua ya kipekee sana ni BARABARA yetu ya PANGANI
kupewa kibali rasmi cha matengenezo toka kwa Mh.Rais wetu Mpendwa Dk.John
Pombe Magufuli na hapa nimefika ofisini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu
Dodoma kujionea na kushukuru.
..
..
Ndugu
zangu kila kilio kina mwenye ,;machozi ya furaha yamenitoka nilipopewa
habari hizi,nimekumbuka mbali sana tulivyoumia, tulivyoteseka pamoja na kwa
miaka mingi sana kusubiri hili.
..
Hisia
zimenipeleka mbali nilivokosa amani toka nilipopata ridhaa ya kua Mbunge namna
nimekosa usingizi kila nikiwaza kulimaliza na kufanikisha hili,nilifikia hatua
kila nikisimama Bungeni nasemea barabara tu,nilipiga mpaka MAGOTI kwa Waziri
Mbarawa alipofika Pangani,nimeenda ofisi zote hamna sehemu sijafika kuisemea
barabara hii,nimetembelea Media mbalimbali.,nimemuomba sana Mungu kila nifapo
Dua.!
..
Leo
ni siku ya kihistoria ninaomba kuwajulisha rasmi kua tunaenda kupata barabara
ya kiwango cha lami na zoezi hili litaanza muda si mrefu.
Tumesema
sana,tumepaza sauti kila kona,tumezungumza na kila aliehusika na sasa faraja
kubwa hii hapa Mbele yetu.!
..
Nichukue
nafasi hii kuwashukuru sana wana Pangani kwa uvumilivu wenu kipindi chote
nilipowaambia naipambania barabara hii,na niwaombe tuendelee kua na subira
mpaka mchakato unapoanza,nawashukuru sana kwa Dua zenu na nawaomba uzidi
kuniombea nina mengi ya kufanya kwa ajili yenu.
..
Mwisho
nikiri nimeupokea utendaji wa Mh.Raisi wetu wa Miaka mitatu kwa moyo wa furaha
sana na Mungu ampe nguvu na Afya na maisha marefu tokana na hiki kilio cha muda
mrefu kinachokwenda kufutika ikiwa ni kama Pangani tulikua pangoni sasa
tunaenda kupaa angani.!
No comments:
Post a Comment