SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

 

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.


Na Athumani Shomari


Bagamoyo.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga amechangia mifuko 50 ya Cement kwaajili ya ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Msingi Sirajulmunir iliyopo kata ya Nianjema wilayni Bagamoyo.


Mkuu huyo wa wilaya ametoa Ahadi hiyo hivi karibuni, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya wahitimu wa darasa la saba, katika shule hiyo.

Akizungumza kwa niaba yake, Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya, Ibrahim Gama amesema juhudi zinazo oneshwa na shule hiyo zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo ndani na nje ya Bagamoyo.


Amesema Watoto wanaosoma Shule ya Sirajulmunir wana uwezo mkubwa katika masomo hali inayopelekea kila mwaka kufanya vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na wanakuwa Watoto wenye maadili mema katika jamii.


Aliongeza kwa kusema kuwa, ufasaha wa lugha ya kingereza, kiarabu, ufaulu mzuri na maadili mema ni Ishara kubwa ya ubora wa elimu inayotolewa shuleni hapo ambayo humjenga mtoto kuwa na nidhamu na utiifu kwa jamii.


Gama amesema Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, inaunga mkono wazo la kuanzishwa kwa shule ya Sekondariy ya Sirajulmunir ili wahitimu wa elimu ya msingi katika shule hiyo waende katika Sekondari yao ya Sirajulmunir ili kuendeleza malezi bora waliyoyapata shuleni hapo.


Ametumia nafasi hiyo, kuipongeza Taasisi ya Sirajulmunir Islamic Centre ambayo ndio inayomiliki shule hiyo kwa usimamizi mzuri wa uendeshaji, pamoja na walimu na wafanyakazi wote wa shule ya Sirajulmunir Bagamoyo kwa juhudi kubwa ya kuwapa Watoto elimu iliyo bora.

Amesema kupitia maonesho mbalimbali ya watoto, ufasaha wa kujieleza na ufaulu mzuri kwao ni miongoni mwa vitu vya kujivunia kwamba ipo juhudi kubwa iliyofanywa na walimu na kwamba wazazi pia wanapaswa kuthamini juhudi hiyo.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Amiri wa Taasisi ya Sirajulmunir Islamic Centre, Sheikh Abdallah Kindamba, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule ya Sirajulmunir ili wapate elimu iliyo bora.


Sheikh Kindamba amesema shule ya Sirajulmunir inamjenga mtoto kupata elimu ya mazingira na elimu ya Mwongozo ambayo itamuwezesha kumjua MwenyeMungu na kujenga hofu katika moyo wake ili akifanikiwa kupa kazi asiwe mbadhilifu wa mali za umma.


Amesema kwa sasa wapo watumishi kwenye sekta binafsi na serikalini ambao wanafanya kazi bila ya kuwa na hofu ya MwenyeziMungu hali inayopelekea kufanya ubadhilifu wa mali ya umma na kutowatendea haki watu wanaowahudumia.


Aliongeza kwa kusema kuwa, shule hiyo inatoa elimu ya maadili na uadilifu kwa kuwafundisha Watoto madhara ya Rushwa, uongo, ufisadi na hujuma ambapo mtoto anafundishwa kuwa akitumwa kazi na Mwalimu wake na asipoifanya, hiyo ni hujuma anamuhujumu Mwalimu wake asifikie malengo yake, na hivyo hivyo anapaswa kuzingatia hata akiwa kwenye ajira atambue kutotekeleza maagizo ya mwajiri wake ni kumuhujumu mwajiri wake jambo ambalo ni baya katika uislamu.


Amiri Kindamba amesema vijana wengi waliopata elimu yao ya msingi Sirajulmunir wameenda kuwa mfano wa kuigwa katika shule za sekondari walizoenda na wakapewa nafasi mbalimbali za uongozi maeneo wanayoenda madarasani n ahata kuongoza ibada za swala mbalimbali.


Alisema mpaka sasa shule inaadhimisha mahafali ya 16 tayari imetoa vijana waliomaliza vyuo vikuu, ndani na nje ya nchi na wengine wakiwa wameajiriwa katika vyuo na shule walizosoma ikiwa ni Ishara ya tabia njema walizonazo.


 “Huwezi kusoma shule au chuo uwe na tabia mbaya kisha wakupe ajira hapohapo, hiyo haiwezekani, kitendo cha vijana wetu kumaliza masomo katika vyuo na shule walizosoma na kisha kupewa ajira katika vyuo na shule hizo ni Ishara ya kuwa na elimu bora na tabia njema”. Alisema Amiri Kindamba.


Akizungumza kwa niaba ya wazazi, mzazi Mustafa Musa Sinzia, amesema wazazi na walezi wa Bagamoyo wanajivunia uwepo wa shule hiyo ambayo licha ya kupata elimu iliyo bora, Watoto pia wanatoka na tabia njema zinazoakisi katika jamii wanazoishi.


Amesemaw apo wazazi ambao wana Watoto zaidi ya mmoja hawatamani tena kupeleka Watoto wao shule nyingine na badala yake Watoto wote wa mzazi mmoja wanapelekwa shule ya Sirajulmunir Bagamoyo.


Akisoma risala ya shule mbele ya mgeni rasmi, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sirajulmunir Bagamoyo, Mapesa Waziri, amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika shule hiyo yenye wanafunzi 320, kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mabweni, bwalo la chakula, uzio, ofisi za walimu, vifaa vya Tehama pamoja na chumba cha Kompyuta. 


Amesema Kipaumbele cha shule hiyo kwa sasa ni kupata bwalo la chakula, ili Watoto wapate sehemu yenye utulivu na salama wakati wakula.


Katika kuchangia ujenzi wa Bwalo la chakula kwa wananfunzi, Jumla ya shilingi Milioni tano zimepatikana siku hiyo ya mahafali ikiwa ni pesa taslimu pamoja na Ahadi.


Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya, Sheikh, Ibrahim Gama, akizungumza katika mahafali hayo.
Amiri wa Taasisi ya Sirajulmunir Islamic Centre, Sheikh Abdallah Kindamba, akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi.
 
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sirajulmunir Bagamoyo, Mapesa Waziri, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Wahitimu wa darasa la saba





Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AKIPEWA POLE NA VIONGOZI MBALIMBALI

SHULE YA MSINGI IPULI YAPEWA TUZO YA UFANISI

THE ISLAMIC FOUNDATION YAMKABIDHI CHEREHANI ALIYEMALIZA KIFUNGO GEREZANI.

MAONESHO YA MADINI YAIPAISHA LINDI KIMAPATO - MAKUSANYO YAFIKIA BILIONI 10.5

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUANZA JANUARI 2027

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU

MWENYEKITI MBEYA DC ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI WA SHULE

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

MUME WA RAIS DKT. SAMIA AFARIKI DUNIA.