Masoud Kipanya, Shishi baby waukwaa ubalozi wa naweza, watoa nasaha nzito kwa wazazi
Mwandishi wetu, Dar es Salaam Imeelezwa kuwa wazazi wanapaswa kujiona ni wenye bahati kwa kupata mtoto na kwamba wanatakiwa kumthamini kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kumpa stahiki zake zote ikiwemo kumnyonyesha kwa miaka miwili bila kumkatisha. Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la mawasiliano la naweza kupitia smart generation, Shilole alisema kuna wanawake wengi sana wamekuwa na tabia ya kikatili ya kumnyima mtoto wake kunyonya kwa muda mrefu, wakihofu usichana wao utakwisha. Alisema jambo hilo sio zuri, kupitia jukwaa la naweza atahakikisha anahamasisha wanawake kuwa na tabia ya kuwathamini watoto wao, waache tabia ya kuwawekea pilipili katika chuchu mara tu inapofika miezi mitatu. “Mthamini mtoto wako, usimkatili mtoto ndani ya miezi mitatu unamnyima ziwa huko ni kumkosea mtoto, lakini pia ni kujitengenezea mtoto ambaye hana akili, anakuwa zezeta,” alisema Shilole. Usiogope kuwa ziwa litadondoka, ukishakubali kuwa mama huna sababu ya kuwaza kuwa ziwa lako linadond...