DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

 

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA



Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, leo ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Kodi ya Wilaya kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.


Kikao hicho kimejadili tathmini ya mwenendo wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kuweka mikakati ya kuimarisha makusanyo kwa mwaka 2026/2027.


Akizungumza katika kikao hicho, Shaka amesema kazi ya kukusanya kodi sio ukusanyaji tu, bali ni ujenzi wa maendeleo.


 "Sisi sio wakusanya kodi tu, bali ni wajenzi wa maendeleo. Kila shilingi tunayokusanya kwa haki na uadilifu, tunajenga kesho bora ya wananchi wetu. Hivyo jukumu letu sio dogo," alisema Shaka.


Aidha, Shaka ameelekeza kila chanzo cha mapato Wilayani humo kipitiwe upya.


"Kile ambacho kimekufa kifufuliwe, kile ambacho kinalala kiamshwe. Lazima tubadili mtazamo kutoka kudhibiti kwenda kuelimisha umma," alisisitiza.


Ameitaka TRA na Halmashauri kuimarisha matumizi ya takwimu halisi (Data) na kufunga mihuri yote ya uvujaji wa mapato.


"Mapato yanayokusanywa lazima yaingie yote. Tunahitaji uwazi wa mifumo ya ukusanyaji wa kielektroniki. Wilaya ya Kilosa ina uwezo wa kukusanya zaidi ya mara mbili ya tunayokusanya sasa, kama watendaji wataamua kuwa wabunifu na waadilifu," alifafanua.


Shaka amemalizia kwa kusema, "Tusiogope kufanya mapitio magumu. Bora kuwa na vyanzo 20 hai vinavyoingiza kuliko kuwa na vyanzo 100 hewa vinavyotupa sifa bandia."


 Naye Katibu wa kikao hicho, Meneja wa TRA Kilosa, Bi. Saada Mtoto, amesema TRA katika kipindi kilichopita imevuka malengo ya ukusanyaji na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa ili kufikia malengo endelevu.





Comments

Popular posts from this blog

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.