Posts

Showing posts with the label SIASA

AFISA ANAYETUMIA CHEO KUOMBA RUSHWA YA NGONO AUMBUKA.

Image
AFISA Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Valintine Mbai ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Halmashauri hiyo ametakiwa kuacha tabia  ya kutumia cheo chake kuomba rushwa ya ngono kwa Watendaji wa Vijiji katika Halmashauri hiyo na  kubadili mwenendo wake haraka iwezekanavyo. Onyo hilo limetolewa na  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa  wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.  Akizungumza na watumishi hao, Mary amesema, ni aibu kwa afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia maadili ya kiutumishi kutumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono toka kwa Watendaji wa Vijiji jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya kiutendaji katika utumishi wa umma. Amemtaka afisa huyo kuacha tabia hiyo na kujirekebisha maramoja ili awe mfano bora kwa watumishi anaowasimamia kimaadili. Pia amemtaka, a...