Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga Bw.
Zachopolous Georgions. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua
ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa
siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za
kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo ya mpango wa kuborsha barabra za Mkuranga kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati)
wakati akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango
cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza
shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani kulia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
moja ya vifungashio vinavyotumika kufungashia vigae vya marumaru (tiles)
alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo
Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment