Meneja
wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka
akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo Pichani) wakati wa Mafunzo
ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko (
Composite Flour)na siagi ya karanga yanayofanyika Jijini hapa.
............................
Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa elimu
kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa
wanazozalisha hususani unga wa mahindi na siagi ya karanga kuwa na vimelea vya
ugonjwa wa sumukuvu ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji na wakati mwingine
husababisha vifo.
Mafunzo hayo yanatokana na ripoti ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa
bidhaa zitokanazo na unga mchanganyiko na siagi ya karanga uliofanywa na
mamlaka hiyo ya mwaka 2015-2018 na kubaini mazo hayo huzalishwa kwa wingi
mkoani humo yana dalili ya uwepo wa fangasi na sumukuvu.
Akizungumza na washiriki Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka
Kessy amesema kuwa wasindikaji wa chakula wanahitajika kuwa wasafi na weledi
mkubwa kwa kuwa kinyume na hapo athari yake ya kupata sumukuvu ni hatari kwa
walaji.
“Katika ufuatiliji huo ilibainika kuwa bidhaa hizi zilikuwa na dalili ya
uwepo wa sumukuvu,hususani katika bidhaa zitokanazo na mahindi na karanga hizi
ndizo wajasiliamali wengi wanauza”amesema Bw.Kessy
Kwa upande wake Meneja wa kanda ya kati Dodoma wa Mamlaka ya chakula na
dawa (TFDA) Dkt Engelbart Bilashoboka,amewataka wasindikaji kubaini vyanzo vya
uchafunzi wa chakula kutokana na sumukuvu ili waweze kuizuia.
Dk.Bilashoboka amesema kuwa wasindikaji wakibaini watakuwa wamewalinda
walaji wa bidhaa hizo zinazotengenezwa kwa kuepusha maradhi kama vile ya kuumwa
tumbo,kutapika,kuharisha na hali ya umanjano machoni na viganjani na hata
kusababisha ba vifo pia.
Aidha amesema kuwa malengo ya mamlaka hii kuanzishwa kwake ni
kuhakikisha kuwa chakula,dawa,vipodozi,vifaa tiba na votendanishi
vitakavyotumika hapa nchini na vinakidhi ubora na usalama kwa watumiaji.
Kwa upande wa baadhi ya Wasindikizaji wamekiri kutokuwa na uelewa juu ya
sumukuvu kwani awali walikuwa wakisindika Nafaka Kienyeji bila kuchagua mazao
ambayo mengine yana dalili za uwepo wa vimelea vya ugonjwa huo.
Washiriki
wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko (
Composite Flour)na siagi ya karanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi
waliokaa kwenye viti kulia ni Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda
ya kati DK.Englbert Bilashoboka na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma
Bw.Maduka Kessy.
No comments:
Post a Comment