Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka Halmashauri nchini kupambana na kudhibiti maambukizi ya malaria ili taifa kuondokana na tatizo hilo na hivyo badala ya kuhangaika – muda na gharama – na matibabu, kutoa nafasi kwa wananchi kuendelea na ujenzi wa taifa wakiwa na afya njema .
Akizungumza katika uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa viashiria vya
malaria nchini, wa mwaka 2017, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka watendaji hao wakuu; wakuu wa wilaya na wakuu
wa halmashauri zote nchini kupambana na maambukizi ya malaria ili kutokomeza
tatizo hilo nchini
“… mwezi Mei, 2015 Kasulu, Kigoma, kwenye maadhimisho ya siku ya malaria
duniani tulizindua takwimu za awali ambazo zilionesha kiwango cha malaria
kimeshuka toka asilimia 14 hadi asilimia 7 huku mikoa ya Kigoma asilimia 24.4,
Geita asilimia ni 17.3, Mkoa wa Kagera asilimia 13.4 na Mtwara asilimia 14.8 …
malaria bado ni kubwa, kwa hiyo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika
halmashauri hizo, wafanye kazi ya kusimamia kazi ya kutokomeza malaria”, Waziri
Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy alisema kuwa katika utafiti huo unaonesha kuwa kila
Halmashauri zina asilimia kadhaa za kiwango cha malaria, kwa maana viwango
hivyo havikatishi tamaa kwa watendaji wa halmashauri kuchukua dhamira madhubuti
ya kupambana na maambukizi ya malaria katika maeneo yao ili kutokomeza kabisa
tatizo hilo, kama mpango wa Serikali wa kupambana na malaria unavyobainisha.
Aidha, Waziri aliongeza kuwa, katika hali ya kudhibiti kiango cha
malaria, Serikali ina mpango wa kushusha kiwango hicho hadi kufika chini ya
asilimia moja ifikapo 2020, kadhalika kutokomeza kabisa malaria ifikapo 2030,
ili kuwawezesha wananchi kufanya kazi wakiwa na afya njema.
“tumeweka malengo kwamba kufikia 2020 tunataka kiwango cha malaria
kifikie chini ya asilimia moja, na ifikapo 2030 tuwe tumetokomeza kabisa
malaria nchni.” Amesisitiza Waziri.
Akaongezea kwa mfano, kwa Mkoa wa Kigoma ambapo halmashauri zake kiwango
ni kikubwa zaidi, zikwemo Halmashauru za Kakonko (asilimia 30.8), Kasulu
(asilimia 27.9), Kibondo (asilimia 25.8), Uvinza (asilimia 25.4), Kigoma
(asilimia 25.1), Buhigwe (asilimia 24) na Kigoma (asilimia 25.1), halmashauri
hizi na nyinginezo, Wakurugenzi pamoja na watendaji wengine eneo la afya na
jamii, wanapaswa kufanya kazi na wananchi ili kuweza kuondoa tatizo hili.
Kwa upande mwingine, wananchi wametakiwa kushirikiana na watendaji wa
Halmashauri kutunza mazingira yao kwa kufukia madimbwi, kujenga vyoo bora, kukata
nyasi na kuzoa taka katika maeneo yao,na kwamba itapunguza vifo
vinavyosababishwa na malaria, kwani takwimu nchini zaashiria vifo vya watoto ni
33 kati ya watoto 1000, wakati Serikali imelenga, kama si kutokomeza vifo, basi
vifikie hadi watoto 9 kati ya watoto 1000.
No comments:
Post a Comment