Friday, October 26, 2018

CHOO CHA SHULE CHATITIA ARUMERU.

Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru limetitia  katika tukio hilo ameokolewa  Mwanafunzi Mmoja wa Kiume aliepata majeraha sehemu na bado  jitahada za kuondoa kifusi kilichochanganyikana na matofali ambacho kimezama katika Shimo la choo kilichokuwa na matundu 20 zinaendelea.



Katika kukabiliana na Changamoto Iliyotokea Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiambatana na Katibu Katibu tawala wa Wilaya na viongozi wa Halmashauri ya Arusha walifika kwenye eneo la tukio na kuanza kazi ya kuratibu jitihada za uokoaji wakishirkiana na vikosi vya uokoji na Zimamoto pamoja na mamia ya wananchi wa kata ya kimnyaki.

Katika shughuli hiyo ya uokoaji walifanikiwa kumuokoa mwananfunzi Mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.

Katika Eneo la tukio kwanza irejeshwa hali ya Amani na kutuliza taharuki za wananchi ambao baadhi Wana watoto wanaosoma katika shule hiyo  vikosi vya ukoaji vinaendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi wengine Kutokana na kutokupatikana kwa Taarifa za awali zinazoonyesha idadi ya Wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.


Awali kwa upande wao baadhi ya wananchi waliungana na Mkuu wa Wilaya katika kuchanga Fedha kwa ajili ya kuanza Mikakati ya Ujenzi wa choo kingine ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa wingi na wananchi waliotoa Fedha zao.

Awali Mhe Muro alilazimika kumtembelea majeruhi ambae amelazwa katika hospitali ya seliani na kumjulia hali uku akiongozana na viongozi mbalimbali.
 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Mhe. Jerry Muro akiwa eneo la tukio kushiriki shughuli za uokoaji.

No comments:

Post a Comment