Monday, October 22, 2018

MBUNGE DKT. KAWAMBWA ASEMA WAKANDARASI WAWILI KUJENGA BARABARA YA MAKURUNGE,SAADANI HADI PANGANI.

 Mbungw wa jimbo Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Gama, Kata ya Makurunge alipokwenda kusikiliza cjangamoto zinazowakabiri wapigakura wake (Hawapo pichani).

Na Omary Mngindo, Makurunge Bagamyo.

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt. Shukuru Kawambwa, amesema kuwa barabara ya Makurunge, Saadani mpaka Pangani Tanga itajengwa na Wakandarasi wawili ili wakazi wote waanze kuona kazi hiyo.

Dkt. Kawambwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Kifude, Kata ya Makurunge jimboni humo, akiwa kwenye ziara ya kupokea changamoto zinazowakabili wapigakura wake, kisha kuziwasilisha katika bunge lijalo.

Ziara ya Mbunge Dkt. Kawambwa iliyoanzia Ijumaa ya Oktoba 19 inayotarajiwa kukamilika Oktoba 30 mwaka huu,  alitoa ufafanuzi huo baada ya mmoja wa wakazi aliyejitambulisha kwa jina la Salum Juma kutaka kujua lini kazi hiyo itaanza, huku akiongeza kuwa wanahamu ya kuona kazi hiyo ikianza.

"Mheshimiwa Mbunge tunataka kufahamu ujenzi wa Barabara inayotokea Makurunge kupitia Saadani, Pangani Tanga lini utaanza?, tunahitaki kuona mabasi yakipitia Barabara hii kwani itatuongezea fursa kiuchumi," alisema Juma.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo, Dkt. Kawambwa alisema kwamba anaimani kubwa kuwa kazi hiyo itafanyika mapema iwezekanavyo, kwa Wakandarasi wawili kufanyakazi kwa wakati mmoja kwa maana ya eneo la Bagamoyo na Pangani Tanga.

"Nilipokuwa bungeni nimemuomba Waziri mwenye dhamana ikiwezekana kuwepo na Wakandarasi wawili wataoanza kazi kwa maana ya kianzia upande wa Bagamoyo na Pangani, akanihakikishia kuwa hilo litawezakana," alisema Dkt. Kawambwa.

Awali Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Stamili Bondo alimweleza Mbunge hiyo kuwa hivi sasa wanaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto hawatembei umbali mrefu, huku akishukuru mchango wa shilingi laki tano kutoka mfuko wa Jimbo.

Akiwa katika Kijiji cha Gama Dkt. Kawambwa amepokea malalamiko ya fidia ya zaidi ya shilingi bilioni moja inayodaiwa kulipwa kwa wananchi awanaotakiwa kupisha mradi wa miwa uliochini unaosimamiwa na Kampuni ya Bagamoyo Sugar.

Baadhi ya wakazi Lukhia Yusufu na Hassan Lingwa kwa niaba ya wenzao wamelalamikia sakata hilo ambao wanedai wengine hawakuingizwa katika tathimini kutokana na kwamba wakati wa zoezi hawakufikiwa kutokana na kuwa kipindi cha mvua.

Dkt. Kawambwa ameahidi kuzichukua changamoto hizo kisha kwenda kuzifikisha kwa viongozi wa ngazi husika kwa lengo la kuzifanyiakazi, huku akiwaomba wanamchi hao kuwa watulivu.
 Wakazi wa Kijiji cha Gama wakimsikiliza Mbunge wao Dkt. Shukuru Kawambwa alipofanya ziara ya siku moja ndani ya Kata ya Makurunge. Picha zote na Omary Mngindo.

No comments:

Post a Comment