Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe
(Mb), amesema habari iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Tanzanite la leo Jumatatu tarehe 29 Oktoba, 2018 lenye
habari zenye tuhuma za kisiasa dhidi ya Viongozi kadhaa, haziakisi msimamo wa
Serikali na ameagiza mmiliki na Bodi ya uhariri ya gazeti hilo waitwe mara moja
Idara ya Habari (MAELEZO) kujieleza kuhusu msingi wa habari hiyo.
Dkt. Mwakyembe ametoa ufafanuzi huo leo mchana, mara baada ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuelezea kushtushwa kwake na
mwenendo wa gazeti hilo kuchapisha habari zinazoibua tuhuma za kisiasa dhidi ya
baadhi ya Viongozi nchini, wakiwemo Wabunge na kusababisha taharuki kubwa
katika jamii.
Gazeti la Tanzanite linatolewa na kampuni ya CZ
Information and Media Consultant LTD ya Dar es Salaam na leo katika toleo lake
Na. 254 limeandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa
kinachosomeka “Vigogo 14 hatari kwa nchi watajwa” ambayo inawataja viongozi kadhaa wa kisiasa
na wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment