MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt.
Shukuru Kawambwa, na Mbunge mwenzake wa Jimbo la Chalinze,
Mwanasheria Ridhiwani Kikwete wakisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati Rais Magufuli alipowasili wialayani Bagamoyo katika moja ya ziara alizowahi kufanya wilayani humo pembeni kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
................................................................
Na Omary Mngindo, Mwavi
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt.
Shukuru Kawambwa, amesema kuwa yeye akishirikiana na Mbunge mwenzake wa jimbo la Chalinze
Mwanasheria Ridhiwani Kikwete wanaendelea kupambana na suala la maji kwa wapigakura
wao.
Dkt. Kawambwa ametoa kauli hiyo katika Kitongoji
cha Vigwaza, Kijiji cha Mwavi Kata ya Fukayosi jimboni hapa, alipokuwa
anazungumza na wapigakura wake inayolenga kupokea chabgamoto zao ili
aziwasilishe kwenye bunge lijalo.
Alisema kwamba mradi wa maji unaosimamiwa na
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) awali ulianza ukiwa
na vijiji 9, sasa kina vijiji zaidi ya mia, ongezeko ambalo limeuzidi uwezo
mradi huo.
"Mimi na Mbunge mwenzangu Ridhiwani Kikwete
upande wa Chalinze kwa pamoja tupo katika harakati za kupambana na tatizo la
maji ambalo limekuwa linawasumbua kwa muda mrefu, niwaombe mtambue hivyo,"
alisema Dkt. Kawambwa.
Aliongeza kwamba awali Serikali iliingia Mkataba na
Kampuni moja ambayo kutokana na kushindwa kutekeleza kazi zake imemfutia
mkataba, hivi sasa iko katika mpango wa kumpata Mkandarasi mwingine
atayeuendeleza mradi huo.
Kwa upande wake mkazi Nuhu Ally alimweleza Dkt.
Kawambwa kuwa, wanatumia muda mwingi kutafuta maji katika visima hali,
inayowapunguzia muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwavi Shabani Mkumbi
alisema kuwa changamoto ya maji kitongojini hapo ni ya muda mrefu, huku
akieleza kuwa wakati wakisibiri mipango ya muda ntefu, ni vizuri kukapatikana
visima vitavyowapunguzia adha hiyo wakazi hao.
Akizungumzia ombi la kisima, Dkt. Kawambwa
amewaambia wana-Vigwaza hao kuwa tayari kuna mmoja wa marafiki zake wapo tauati
kuchimba kisima kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment