Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akifafanua hali ya upatikanaji wa dawa nchini kwa wajumbe wa kamati ya
Bunge ya Huduma za jamii nchini hawapo pichani wakati wa kikao cha kamati ya hiyo
kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
katikati aliyekaa ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.
.....................................
1.
WAMJW,
BUNGENI DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeainisha dawa aina
135 kama dawa muhimu na za kipaumbele cha wizara kwa lengo la kuhakikisha
kuwa zinapatikana nyakati zote katika bohari zote za kanda za MSD.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Janii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa ya
utendaji ya Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) aliyowasilisha katika kamati ya
kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.
Waziri Ummy alisema tathimini ya upatikanaji wa dawa
hizo ni wa hadi mwezi Julai 2018 ambapo ni sawa na asilimia 93 hivyo
Wizara yake imeitaka MSD kuongeza idadi ya dawa muhimu 177 na kufikia
dawa za kipaumbele 312 ambapo upatikanaji wa dawa hizo ni asilimia 73 kufikia
robo mwaka ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.
“Hali ya upatikanaji dawa muhimu umeimarika
kuanzia mwaka 2016/2017 na kufikia asilimia 93 nchi nzima katika mwaka
2017/2018 na hivyo kuweza kufanikiwa katika maeneo mengi na kufikisha
dawa moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za afya nchi
nzima”.Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, Waziri Ummy alisema MSD imeweza kusambaza
dawa moja kwa moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya vinavyofikia 5,432
nchi nzima kwa kutumia magari 215 na hivyo kusambaza dawa zenye thamani
za shilingi bilionini 600 kwa mwaka kupitia mfumo wa ugavi ulio enea nchi nzima.
Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa hivi sasa MSD
inapeleka dawa mara 6 kwa mwaka na pale kwenye mahitaji ya dharura tofauti na
zamani ambapo ilikua inapeleka dawa mara nne kwa mwaka.
Mbali na hayo Waziri Ummy alisema Bohari ya dawa
imeendelea kuimarika kifedha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hususan
katika mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo Serikali iliongeza bajeti ya dawa, vifaa
na vifaa tiba na kuweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 80.1 na kwa
mwaka wa bajeti 2018/2019 kwa robo hii ya mwaka imepokea shilingi bilioni 20.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wafamasia wote
wa Hospitali na vituo vya afya kupeleka orodha ya dawa zilizopo kwenye
stoo kwa madaktari kila mwanzo wa wiki.
“Wafamasia wote wa Hospitali na zahanati za Serikali
wanatakiwa kuwapelekea madaktari orodha ya dawa zilizopo kwenye stoo ili kama
dawa ya ugonjwa Fulani haipo Daktari awe na uwezo wa kuandika dawa mbadala kwa
mgonjwa” amesema Dkt. Ndugulile.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa nchini Bw.
Laurean Bwanakunu amesema kuwa katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa unadumu
nchini wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha ubia kati ya Serikali na
Sekta binafsi kujenga kiwanda cha dawa nchini.
“Tunatarajia mpaka kufikia Machi 2019 kukamilisha
ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi kujenga kiwanda cha dawa nchini ambapo
utafanyika kwa haraka ili kukamilikia mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2019”
alisema Bw. Bwanakunu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akichangia mada wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za
jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania , wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw.
Peter Serukamba akitoa mwongozo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za
jamii nchini wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika
ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,wa kwanza kulia ni Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Katibu
Mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya aliyesimama akichangia mada
wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea
katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , waliokaa
kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu na katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.
No comments:
Post a Comment