Friday, October 26, 2018

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI KAGERA

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera wanatarajia kutoa huduma ya kliniki ya Moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) katika Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 11 Novemba, 2018.

Huduma tutakazozitoa ni pamoja na upimaji wa vihatarishi vya Magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, na kutoa rufaa kwa wananchi watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitajika kupewa rufaa kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.

Matibabu ya kliniki ya moyo inayotembea ni matibabu endelevu yanayolenga kuhakikisha kuwa wagonjwa wa Moyo waliopo mikoani wanapata huduma bora ya matibabu ya Moyo na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo.

Wananchi wote wa Mkoa wa Kagera pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ili muweze kupata huduma za uchunguzi za matibabu ya Moyo.


No comments:

Post a Comment