MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani Ridhiwani Kikwete akiwa makaburini, akiungana na wasanii mbalimbali kumzika msanii Mashaka.
Na Shushu Joel, Dar.
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani Ridhiwani Kikwete ameungana na wasanii wa kada mbalimbali katika kumzika
msanii maarufu wa maigizo nchini Ramadhani Ditopile aliyewai kuwa msanii wa
kundi la sanaa la kaole.
Mashaka alifariki juzi asubui wakati akiwa anapata
matibabu katika hospital ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Ridhiwani alisema kuwa
pengo la msanii huyo ni ngumu kuliziba kwa kipiondi hiki kutokana na jinsi
alivyokuwa akifanya kazi zake kwa weredi.
“Mashaka alikuwa si msanii tu kwangu bali alikuwa ni
mjomba wa mfano kwani alikuwa akinipatia ushauri mkubwa juu ya kazi zangu za
siasa hivyo nimepoteza mtu wa muhimu sana kwangu”Alisema Ridhiwani.
Aliongeza kuwa anawapongeza wote waliofika katika
kuhakikisha tunamzika ndugu yetu,kwani maziko ni wajibu wetu sote kwani ni
ibada.
Aidha mbunge huyo alisema kuwa marehemu mashaka
atakumbukwa kwa kupitia kipaji chake cha uigizaji ambapo katika uhai wake
aliwai kutamba na kundi la kaole kupitia tamthilia za mambo hayo,kidedea,jumba
la dhahabu na nyingine nyingi.
Kwa upande wake msanii maarufu wa uigizaji nchini Mzee
chilo alisema kuwa Mashaka alikuwa ni mtu wa pekee katika tasinia ya kuigiza kutokana
na kupenda kutumia kipaji chake kuwaelekeza wenzake pindi mnapokuwa katika
kazi.
Aliongeza kuwa ni pengo kubwa katika fani yetu lakini
kutokana na kuwa hapa duniani tunapita hakuna budi kumuombea kwa Mungu ili
apumzike kwa amani.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Abdallah Ditopile,baba
yake aliugua ghafla usiku wa kuamkia juzi na kisha kupelekwa hospital ya Amana
ambapo alilazwa kabla ya kufariki akiendelea kupatiwa matibabu.
Aidha alisema kuwa baba yake alizidiwa na kupewa rufaa ya
kwenda mloganzila lakini wakiwa wanasubili gari ili waelekee huko baba
alipoteza maisha”Alisema Abdalaah.
Aliongeza kuwa anawashukuru watnzania wote waliojitokeza
kwenye makaburi ya kifamilia yaliyoko Tabata Kinyelezi kwa ajili ya kumzika
baba sina la kuwalipa ila Mungu atawalipa kwa wema mliotufanyia wanafamilia.
No comments:
Post a Comment