Blog ya
BAGAMOYO KWANZA yapata usajili na kukabidhiwa leseni itakayowawezesha kuendelea
kutoa huduma za kutoa Habari kwa njia ya mtandao.
Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali kupitia Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) lililotolewa Tarehe 20 April 2018 limewataka wamiliki
wa Blog, Majukwaa ya mtandaoni (Online forums) Radio na Televisheni za
mtandaoni kufanya usajili na kupatiwa leseni itakayowaruhusu kutoa huduma kwa
njia za mtandao.
Usajili wa Blog, Majukwaa ya mtandaoni, (Online
forums) Redio na Televisheni za mtandaoni unafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 4 ya
Maudhui Mtandaoni ya Mwaka 2018 (The Electronic Postal Communications (online
content) Regulations, 2018) ambapo TCRA imepewa dhamana ya kuandaa na kutunza Rajisi
ya watoa huduma za maudhui kupitia Blogu, Majukwaa mtandaoni (online Forums), Redio
na Televisheni mtandaoni, ili kudhibiti na kuchukua hatua panapotokea ukiukwaji
wa Kanuni hizo.
Hivi ndio vyeti vinavyokuwezesha kumiliki Blog Tanzania.
Hivi ndio vyeti vinavyokuwezesha kumiliki Blog Tanzania.
No comments:
Post a Comment