Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe
akisoma kijarida cha Hifadhi ya Taifa ya Saadani alipotembelea banda la
maonesho la Hifadhi hiyo katika Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo alipokuwa analifunga rasmi Oktoba 20,2018. Kulia ni Mhifadhi Utalii wa Saadani Bi. Apaikunda
Mungure.
………………….
Ofa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa Tsh 91,000 tu
BAGAMOYO:
Hifadhi ya Taifa ya Saadani kupitia Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo limetangaza ofa kwa Watanzania na wasio Watanzania kutembelea hifadhi hiyo
kuanzia Oktoba 25, 26 na 27 mwaka huu kujionea vivutio mbalimbali vya Utalii.
Akizungumza Mhifadhi Utalii, Hifadhi ya Saadani, Bi. Apaikunda Mungure
alisema ofa hiyo ni maalum kwa msimu huu wa tamasha la Sanaa Bagamoyo
ambapo kwa kiasi cha Tsh. 91,000 ni gharama kwa Raia wa
Tanzania pamoja na Afrika Mashariki huku wageni kutoka nje ya Afrika Mashariki
hao watalipia US$120 tu.
“Ofa hii itanda kwa muda wa siku tatu. Oktoba 25, 26 na 27.
Wageni wataenda Saadani na kurudi hapa Bagamoyo. Kwa kiasi hicho cha Tsh.
91,000 inajumlisha usafiri wa magari ya Kitalii, usafiri wa kuzunguka na boti
kwenye makutano ya Mto Wami na bahari ya Hindi.
Pia watapata kifungua kinywa, chakula cha mchana na vinywaji na kutembelezwa
kwa safari za kuangalia wanyama na magari” alieleza Bi. Apaikunda
Mungure.
Ameongeza kuwa kwa familia itakayokuwa na motto atamlipia Tsh. 71,000.
Saadani ni hifadhi ya kipekee ambapo Nyika na bahari
vinakutana pamoja. Ndani ya hifadhi hiyo ina aina mbalimbali za wanyama pori,
fukwe ya bahari ya hindi.
Iko katika mkoa wa Pwani na Tanga
Watanzania ambao wapo Bagamoyo na miji jirani ya Dar es Salaam ni fursa
ya kujitokeza kwenda kujionea Utalii wa ndani wenye kila aina ya vivutio vya
Wanyama na safari zitakuwa kila siku kwa wageni kuanzia saba ambao wao kila
mmoja atakaa kwa siti tena dirishani (window seat).
No comments:
Post a Comment