Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea
zawadi maalum ya kumpongeza kwa kufanya ziara yenye mafanikio mkoani Pwani toka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) mara baada ya
ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
....................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan ametoa rai kwa Watanzania kupenda vya kwao kwa kujenga Utamaduni wa
kutumia bidhaa zinazozalishwa nyumbani.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Hafla ya Ufunguzi wa Wiki ya
Viwanda mkoani Pwani.
“Natoa wito kwa jamiikujenga utamaduni wa kutumia bidhaa zilizozalishwa
kwenye viwanda vyetu ndani ili viweze kuendelea kwa kuwa tusipofanya hivyo
viwanda vinavyojengwa havitaedelea na nchi yetu kubaki masikini pamoja na
wananchi wake” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais ambaye amekuwa kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha
shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani amefahamishwa kuwa mkoa huo una viwanda
takribani 429 vikiwemo vikubwa vya kati na vidogo.
Kauli Mbiu ya Maonyesho hayo ni “Viwanda Vyetu, Uchumi wetu Pwani
Tumeweza Tunatekeleza na Tunakuza Uchumi wa Viwanda”.
Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa mkoa kubuni onyesho hilo na kulitaka
liwe endelevu na pia alipongeza Wizara ya Nishati, Dawasa pamoja na Shirika la
Reli kwa kuwa na mkakati maalum wa kuwafikishia huduma hizo wenye viwanda.
Makamu wa Rais pia aliwapa angalizo wazalishaji wa bidhaa zinazofanana
kutochafuana kibiashara badala yake waache bidhaa zao zishindane zenyewe
sokoni.
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amempongeza Makamu
wa Rais kwa kufanya ziara ya siku sita mkoani humo na kuwafungulia maonyesho ya
Viwanda na kuahidi mkoa wake utaendelea kuwa pokea wawekezaji wa viwanda na
kuhakikisha wanafanikisha taratibu zao kwa haraka zaidi.
Hitimisho ; Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano amemaliza ziara yake ya
kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Pwani na kuwataka viongozi
hao kufanya kazi kwa kushirikiana na kuelewana katika kuleta ufanisi kwenye
kazi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosamara baada ya kutembelea banda la
kampuni inayotengeneza reli mpya ya kisasa ya YAPI MERKEZ wakati wa ufunguzi wa maonyesho
ya wiki ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela cheti ya Udhamini Mkuu wa maonyesho ya
Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela Tuzo ya Udhamini Mkuu wa
maonyesho ya Viwanda mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wadhamini wa maonyesho ya Wiki ya Viwanda
mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment