MKUU wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
..............................
Na Ahmed Mahmoud Arusha.
MKUU wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,ameziagiza halmashauri zote saba za
mkoani Arusha, kuhakikisha wanadhibiti matukio ya mimba kwa wanafunzi wa
shule za sekondari na msingi, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale
wote waliowatia mimba wanafunzi hao.
Gambo,ametoa agizo hilo Oktoba 27 kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya
mkoa,RCC, na kueleza kusikitishwa kwake na wanafunzi hao kukatishwa masomo
kutokana na uja uzito.
Ameagiza kuhakikisha utoro shuleni unadhibitiwa sanjari na wazazi
kuhakikisha wanachangia chakula shuleni ili kuwezesha wanafunzi kuwa na umakini
kwenye masomo yao na hiyo pia ni njia ya kupunguza utoro.
Gambo,amempongeza ,mmiliki wa kiwanda cha Mount Meru Millers,ambae
ameahidi kutoa chakula cha mchana kwa shule zote za msingi jijini
Arusha,amekuwa akitoa chakula bure kwa wanafunzi 2000 wa shule za msingi jijini
Arusha.
Akizungumzia ufaulu wa matokeo ya darasa la saba mwaka huu ambapo mkoa wa
Arusha umeshika nafasi ya tatu kitaifa,Gambo,amesema mafanikio hayo yanatokana
na mkakati wa kusimamia na kufuatilia maendeleo ya elimu ikiwa ni pamoja na
shule zote kufanya mtihani mmoja wa pamoja.
Amesema kuwa wamekubaliana na mkoa wa Dar es Salaam kuwa na mtihani
wa pamoja, pia kushindanisha shule za msingi za mkoa wa Arusha na Dar es
Salaam,
Gambo,amesema hiyo ndio siri ya mafanikio kwa mkoa wa Dar es Salaam
kuongoza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu ingawa baadhi ya
shule zimekuwa na madowa katika matokeo hayo ,lakini Arusha iko salama kutokana
na kuwa na uadilifu
Amekiri kuwa matokeo yamekuwa na changamoto za ukosefu wa vyumba vya
madarasa na kuahidi kuwa hadi January mwakani shule zitakapofunguliwa vyumba
hivyo vitakuwa vimeshajengwa na kukamilika.
Hata hivyo serikali kuvifungia vyuo na shule zisizosajiliwa
SERIKALI imesisitiza msimamo wake wa kuzifungia shule za awali,msingi na
vyuo ambavyo havijasajiliwa ikiwa ni hatua ya kudhibiti elimu isitolewe
kiholela bali kwenye maeneo maalumu yenye sifa.
.Kauli hiyo imetolewa Oktoba 27 na Naibu waziri wa Elimu, William ole
Nasha, MB, alipokuwa akichangia kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa
Arusha,RCC, na kusisitiza kuwa taasisi zote za elimu lazima zisajiliwe
vinginevyo hazitaruhusiwa kutoa huduma ya elimu nchini.
Nasha,ambae pia ni mbunge wa jimbo la Ngorongoro,mkoani Arusha,Kuhusu
ufaulu wa darasa la saba mwaka huu,amepongezamkoa huo kwa ufaulu huo na kueleza
kuwa siri ya kupata matokeo mazuri ni mkakati wa mkoa wa kuwa na mtihani mmoja
kwa shule zote za msingi pia usimamizi na ufuatiliaji .
Amesema ufaulu umepanda kutoka asilimia 72.7 mwaka jana hadi kufikia
asilimia 77.7 huku wilaya ya Longido ambayo ilikuwa ikishika mkia kwa miaka
iliyopita ufaulu wake umefikia asilimia 85 hivyo kuvuka lengo la kitaifa ambalo
ni asilimia 77 na imekuwa ni wilaya ya tatu mkoani humo.
Kuhusu usimamizi wa miradi, Waziri, Nasha, amesema lazima miradi
yote inayotekelezwa kwa fedha za serikali ikamilike kwa ubora uliowekwa na
ndani ya muda ,akawataka wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanaisimamia
ipasavyo.
Kuhusu upungufu wa walimu wa sayansi,hisabati amesema serikali
mwakani itaajiri walimu wengi lengo ni kutosheleza mahitaji na walimu
wanaoajiriwa wanagawanywa kwenye shule kulingana na uwiano na mwaka huu
serikali imeajiri walimu 7000
Amesema bado kuna upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya
sayansi,hisabati na Tehama ni mkubwa na serikali itaendelea kuwaajiri ili
kukabiliana na upungufu huo..
Kwa upande mwingine
SERIKALI imetoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa hospital
mbili za wilaya za Longido na Ngorongoro mwaka huu 2018,ikiwa ni hatua ya
kuboresha huduma ya afya na kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Arusha,Dakta Omari Chande, ameyasema hayo
Oktoba 27wakati akiwasilisha taarifa ya huduma ya afya kwenye kikao cha kamati
ya ushauri ya mkoa RCC, na kusema kuwa kila wilaya imepewa shilingi milioni 500
kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa hospital hizo za wilaya.
Dakta,Chande,amesema kuwa mkoa umefanikiwa kutoa chanjo ya mlango
wa kizazi kwa wasichana asilimia 80% na chanjo ya pili itatolewa Novemba
mwaka huu Kuhusu upatikanaji wa dawa amesema kiwango cha upatikanaji wa dawa ni
asilimia 94% .
KKuhusu watumishi,Dakta Chande, amesema mkoa una
upungufu wa watumishi wa afya wa kada mbalimbali, hivyo halmashauri
zinapaswa kuomba Wizara ya Utumishi watumishi hao kwa kuzingatia kada zao .
Akiwasilisha taarifa ya elimu, afisa elimu mkoa wa Arusha,Gifty
Kyando,amesema Mkoa una upungufu wa vyumba 413 vya sekonbdari huku jiji
la Arusha likiongoza kwa upungufu wa vyumba 192, ArushaDC vyumba 109, Meru
vyumba 37 Monduli vyumba 32 Longido vyumba 29 na Ngorongoro vyumba 33 isipokuwa
wilaya ya Karatu ndio pekee isiyokuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa.
Amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni mimba kwa wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari,ambapo jiji la Arusha linaongoza kwa wanaunzi kupata mimba
.
Jumla ya wanafunzi 38293 walisajiliwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu
ya msingi, na waliofanya mtihani ni 37,820 ,waliofaulu ni 33035 sawa na
asilimia 87.30 huku jiji la Arusha likiongoza kwa kufaulisha ambapo mkoa
umekuwa wa tatu katikitaifa katika kufaulisha wanafunzi mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment