Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya
Iringa vijijini Marco Kihongo (kushoto) akipokea msaada wa
fedha kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya ununuzi wa
kadi za chama ,kutoka kwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif
Abri
...............................................
JUMUIYA ya wazazi wa chama cha mapinduzi
(CCM) wilaya ya Iringa vijijni mkoani Iringa
kimepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na mjumbe wa
mkutano mkuu wa CCM Taifa anayewakilisha wilaya ya
Iringa vijijini Arif Abri katika kuiwezesha jumuiya
hiyo kuwa na miradi yake .
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Marco Kihongo ametoa
pongezi hizo leo wakati akipokea pesa
kiasi cha shilingi milioni 1 kutoka kwa mjumbe huyo kwa ajili ya kutekeleza
ahadi yake aliyoitoa kwa jumuiya hiyo ya
kuchangia pesa hizo kwa ajili ya ununuzi wa kadi za jumuiya
kwa wanachama wapya.
Kihongo alisema kuwa mchango huo wa fedha ni
mtaji mkubwa kwa jumuiya hiyo kuweza kuongeza idadi kubwa
zaidi ya wanachama wake na kuwa zoezi la
uongezaji wanachama litaanza mara moja kuanzia sasa .
Huku katibu wa jumuiya hiyo Martin
Mfala alisema pamoja na mjumbe huyo kuchangia kiasi
hicho cha fedha pia aliwaagiza kutafuta mashamba
kwa ajili ya kupanda miti pamoja mbali mbali
ikiwemo ya korosho katika tarafa ya Idodi na kuwa
tayari wamefanikisha kupata ardhi kwa ajili ya kununua na
kukodi kwa kupanda miti hiyo .
Hivyo alisema iwapo watafanikiwa kupata
ardhi hiyo wataweza kupanda miti ambayo itakuwa ni sehemu ya miradi
ya jumuiya ya wazazi katika wilaya hiyo huku
akiomba kusaidiwa kutengeneza pikipiki mbili za jumuiya hiyo
ambazo kwa sasa ni mbovu kwa ajili ya kusaidia
usafiri wa kwenda kutembelea miradi ya jumuiya .
Awali mwanachama wa CCM wilaya ya Iringa vijijini
Thom Malenga ambae ni katibu wa mbunge wa jimbo la Ismani ,Wiliam Lukuvi
alisema kuwa jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa
na Arif Abri katika wilaya ya Iringa ni mfano wa kuigwa
na kuwa kazi mbali mbali amekuwa akichangia hivyo
kuchangia fedha hiyo ni mwendelezo wa misaada mbali mbali ambayo amekuwa
akitoa.
” Tunaamini Mungu humjalia zaidi yule
anayetoa kwa ajili ya wengine kifupi tunashukuru
sana kwa misaada mbali mbali ya kijamii na chama
katika wilaya ya Iringa vijijini ” alisema Thom .
Akikabidhi fedha hizo Arif alisema
pamoja na kuwa amefanya kazi na makatibu wengi wa
wilaya ndani ya wilaya ya Iringa vijijini ila utendaji
kazi wa katibu Dodo Sambu ambaye kwa sasa ni mstaafu
amekuwa mchapakazi sana na kw muda wa miaka mitatu
aliyokuwepo Iringa kazi yake imeonekana.
Hivyo amesema mategemeo yake ni kwa katibu
ajaye kuendeleza umoja na mshikamano uliokuwepo kamanguvu
ya ujenzi wa chama hicho katika wilaya ,mkoa na Taifa
ili ushindi wa CCM uzidi kuongezeka daima.
” Jana wakati namtafuta katibu wa jumuiya ya
wazazi nilimpigia mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Iringa vijijini ambae pia aliomba kusaidia
pikipiki nilimuahidi kuwa asiwe na hofu nitampa
pikipiki hiyo nilitegemea leo kuja kukabidhi hapa ila
kasema yupo nje ya mji kikazi sasa akirudi nitamkabidhi
” alisema Arif
Kuwa maombi ya jumuiya ya wazazi kuhusu kutengenezewa
pikipiki mbili atayafanyia kazi haraka pamoja na
utengenezaji wa gari la chama wilaya .
Mjumbe huyo pia alisema juu ya mradi wa shamba atalitekeleza
kwa kununua shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 20 kama
mradi na kuwa pamoja na miradi hiyo pia umoja wa
wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Iringa nao
watasema wanahitaji nini ili wasaidiwe .
” Nataka kuwaeleza kuw katika familia yangu
mimi kutoka babu zangu wote ni CCM na tunaipenda sana
CCM na tupo tayari kuendelea kusaidia uhai wa chama ili
kuona CCM inaendelea kutawala daima” alisema Arif Abri .
Akishukuru kwa misaada hiyo katibu mstaafu wa CCM
wilaya ya Iringa vijijini Dodo Sambu alisema kuwa
heshima na ushindi wa CCM wilaya ya Iringa vijijini na
mjini imetokana na jitihada za mjumbe huyo wa mkutano mkuu wa CCM
Taifa kupitia wilaya ya Iringa vijijini pamoja na mjumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) anayewakilisha mkoa wa Iringa Salim Asas
ambao wamekuwa wakijitoa kwa nguvu zote .
No comments:
Post a Comment