Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Engineer Evalist Ndikilo
kuhusu masuala Afya pamoja na Maendeleo ya Jamii mapema leo ofisini kwake
Kibaha Mkoani Pwani.
.........................................
Serikali imezitaka Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinakuwa na
vituo vya huduma za mkono kwa mkono (Ones Stop Centre) ili kuunga mkono
serikali katika juhudi zake za kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.
Hayo yamesema leo wilayani kibaha mkoani Pwani na Naibu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
alipotembelea kituo cha huduma za mkono kwa mkono kilichopo katika hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Pwani.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa lengo la vituo hivyo linalenga kupunguza
mlolongo wa huduma kwa muhanga wa ukatili kwani vituo hivyo vinatoa huduma za
matibabu, huduma za polisi na ushahuri wa kisaikolojia kutoka kwa Afisa Ustawi
wa Jamii kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema nchi kwa sasa ina vituo kumi tu hivyo
kutaka maeneo Mikoa mingine kuiga Mkoa wa Pwani kuunga mkono juhudi hizi kwa
kuwa takwimu zilizopo zinaonesha Tanzania ina matukio ya ukatili 41,000 na
kati ya matukio hayo 13,000 ni ukatili dhidi ya watoto akitaja hali hiyo kuwa
ni ujambazi mpya dhidi ya binadamu.
Amezitaja juhudi nyingine za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
kwa wanawake na watoto kuwa ni kuwepo kwa madawati ya Jinsia katika vituo vya
polisi akitaja idadi ya vituo hivyo kote Nchini kuwa ni jumla ya madawati 500.
Ameongeza kuwa Serikali inawajengea uwezomwalimu wa Shule za Msingi na
Sekondari ili kuwa na madawati ya ukatili wa kijinsia kwani vitendo vingi vya
ukatili kwa watoto vinatokea katika eneo la shule.
Dkt. Ndugulile pia ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili
vinavyotokea katika maeneo yao hasa nyumbana katika familia na amesema Serikali
itawachukulia hatua watoa huduma za fya watakaojihushisha na uitoaji wa taarifa
za uongo kuhusu mashauri ya vitendo vya ukatili.
‘’Baadhi ya wanajamii hapa nchini wanafurahia vitendo vya ukatili kwani
wamekuwa wakimalizana kifamilia na kusababisha vitendo hivi kuendelea”
alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri Ndugulile ameuagiza Mkoa wa Pwani pamoja na mikoa mingine
Nchini kuanzisha dawati la ulinzi wa wanawake na watoto akiongeza kuwa ili ni
agizo la serikali hivyo ni lazima mikoa yote Nchini inakuwa na madawati haya
ili kutekeleza agizo la serikali.
Akiongea na watumishi wa hospitali ya Tumbi Dkt. Ndugulile amesema
kumekuwepo na kasumba ya adaktari ya kuficha ushahidi kwa watu
waliofanyiwa vitendo vya ukatili na kuongeza kuwa hilo ni kosa kisheria na
atakayebainika kuficha ushaidi adhabu yake ni kufutiwa usajili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile yupo katika ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Pwani
anmbapo anatembelea na kukagua huduma za afya na maendeleo ya jamii.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile pamoja na Mkurugezi Mkuu wa hospitali ya Tumbi Dkt. Edward Wayi
akitoa maelezo ya Kituo cha Mkono kwa Mkono (one stop centre) kwa waandishi wa
habali kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia mapema leo Tumbi Kibaha Mkoani
Pwani.
No comments:
Post a Comment