MOHAMMED DEWJI APATIKANA AKIWA HAI.

Hatimae Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Dewji amepatikana na amerejea nyumbani kwake kuungana na familia yake akiwa salama. Kwa mujibu wa mtandao wa Makampuni ya Mohamed Enterprises ya MeTL Group, Mo amerejea nyumba ikiwa ni siku ya tisa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana Alhamis Oktoba 11 katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam.

Akitoa taarifa hizo kuptia mtandao wa Twitter unaomilikiwa na Kampuni yake ya Mohamed Enterprises Ltd, Mo ameandika: “Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji na , taarifa ambayo aliipost Saa 9:15 alfajiri, saa za Tanzania.

Aidha, Waziri wa Mazingira, Mhe. Januari Makamba, nae kupitia mtandao wake wa Twitter, amethibitisha kupatikana kwa Mo na kusema kuwa Mfanyabiashara huyo alitupwa maeneo ya Gymkhana huku akiwa na alama za kufungwa kamba mikononi.

“Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri.,” ameandika Makamba.


Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU