MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilaya
ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Malivundo Kata ya Pera katika Jimbo la lake.
...........................
Na Omary Mngindo,CHALINZE.
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilaya
ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete, amewataka viongozi ngazi
mbalimbali kuendelea kufanyakazi kwa pamoja, lengo kuwaondolea changamoto
inayowakabili wananchi.
Ridhiwani ametoa rai hiyo akiwa katika
Kitongoji cha Malivundo Kata ya Pera, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
wapigakura wake waliolalamikia kutokamilika kwa miradi iliyoanzishwa kwenye
eneo lao.
Akiwa katika kitongoji hicho, wananchi walilalamikia kutomaliziwa kwa
zahanati, na shule ambazo tangu ziibuliwe mpaka sasa hazijaendelezwa kwa maana
ya kubaki kama magofu.
"Hapa katika eneo letu kuna
miradi ya zahanati na shule ambazo tangu ziibuliwe na kuanza mchakato wake,
mpaka sasa hazijaendelezwa, kero kubwa sekta ya afya," alisema Juma Issa.
Akizungumzia hilo, Ridhiwani
alielezea masikitiko yake ya kutoendelezwa kwa miradi hiyo, ambapo kwa upande
wake ahadi alizoziahidi amezitekeleza, akiitaja mifuko 50 ujenzi wa zahanati,
mifuko 20 kwenye sekta ya elimu, sanjali na kujenga ofisi.
"Binafsi ahadi ambazo
nimeziahidi nimezikamilisha, niliahidi saruji kifuko 50 ya ujenzi wa zahanati
nimeleta, mifuko 20 upande wa elimu nimekabidhi pia niliahidi kujenga ifisi ya
kijiji ile pale imekamilika, iliyobaki ni ahadi za kiilani ambazo zinaendelea
kufanyiwakazi," alisema Ridhiwani.
Aidha alisema kuwa zahanati hiyo
ataisimamia na kwamba itakamilika kabla ya mwaka 2020, huku akigusia umeme na
miundombinu ya Barabara kutokea njiapanda ya kwa Mwarabu mpaka Malivundo.
Mkazi Idd Fuko wa Kitongoji cha
Pingo alilalamikia kusuasua kwa umaliziwaji wa zahanati ya Pingo, ambapo
alisema wamepata taarifa kwamba kimetengewa kiasi cha shilingi milioni 10
lakini kimesimama kwa muda mrefu pasipokumaliziwa.
Akijibia hill, Ridhiwani alisema
kwamba zahanati hiyo itakamilika kabla ya 2020 na kuanza kazi ya kuhudumia
wananchi, huku akiongeza kuwa kukamilika kwake kutasaidia kupunguza vifo
vinavyotokana na ajali kwenye maeneo hayo.
"Kukamilika kwa zahanati ya
Pingo kutasaidia kupunguza Vigo vya watu wanaopatwa na ajali, kikianzakazi
kutakuwepo na huduma yaa kwanza ambayo kwa kiasi kikibwa kitaweza kusaidia
kupunguza vifo," alimalizia Ridhiwani.
Wananchi wa kitongoji cha Malivundo kata ya Pera
wakati wakimsubiri Mbunge kabla ya kufika ambapo alifika na kuwahutubia.
Picha zote na Omary Mngindo
Picha zote na Omary Mngindo
No comments:
Post a Comment