Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
pamoja na Katiba ya Chama mgombea wa CCM nafasi ya Uwakilishi Jimbo la
Jang`ombe Bw. Ramadhan Hamza Chande wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa
Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa
Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.
......................................
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa
kampeni jimbo la Jang`ombe ambapo Chama Cha Mapinduzi kimemsimamisha Bw.
Ramadhan Hamza Chande kugombea nafasi ya Uwakilishi katika jimbo hilo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, Makamu wa Rais amewataka wakazi wa
Jang`ombe kufuata nyayo walizoachiwa na Wazazi wao.
Mheshimiwa Samia amewambia wakazi wa jimbo hilo kuwa atatoa ushirikiano
wa kutosha kwa kufanya kazi pamoja na Viongozi wa Jimbo hilo katika kuboresha
huduma za afya na elimu.
Pamoja na Viongozi wengine Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mbunge mteule
wa jimbo la Liwale kutoka mkoani Lindi Bw. Zuberi Kachauka ambaye aliwaambia
wakazi wa Jimbo la Jang`ombe kuwa upinzani umekufa kwa kukosa sera na viongozi
bora.
Kampeni za Uwakilishi jimbo la Jang`ombe zilianza tarehe 14 Oktoba na
zinatazamiwa kukamilika tarehe 25 Oktoba 2018 na tarehe 27 Oktoba
wananchi watapiga kura kumchagua Mwakilishi wa jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment