Saturday, October 20, 2018

POLISI KISHAPU YAKABIDHIWA GARI JIPYA KUTOKA MGODI WA MWADUI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akitoa maelekezo na kumkabidhi funguo na kadi ya gari Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kishapu, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Emmanuel Galiyamoshi. Anayeshuhudia kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Alchelaus Mutalemwa.
...................................................

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga limepokea gari jipya kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake kutoka mgodi wa almasi wa Mwadui.


Gari hilo aina ya Nissan Hilux lenye thamani ya sh. milioni 80 limepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack ambaye alikabidhi jeshi hilo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo yaliyofanyika wilayani humo Mhe.Telack aliushukuru mgodi kwa msaada huo.

Telack ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa alisema kuwa gari hilo litawezesha shughuli za Polisi kufanyikaa kwa ufanisi.

Aliwaomba wasichoke kuendelea kuisaidia Kishapu pamoja na kushirikiana na Serikali ya wilaya hiyo kwani wao pia ni sehemu ya jamii hiyo.

Aidha alilitaka jeshi hilo kulitumia gari hilo walilokabidhiwa kwa matumzi yaliyokusudiwa ya kulinda wananchi ili waendelee kuwa na imani nalo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiliangalia gari alilokabidhiwa kwa ajili ya Jeshi la Polisi wilayani Kishapu.

Sehemu ya Askari wa Jeshi la Polisi wilayani Kishapu wakiwa katika furaha baada ya kushuhudia makabidhiano ya gari.  

No comments:

Post a Comment