Mbunge
Ridhiwani Kikwete akimkabidhi Cheti cha ufaulu bora wa somo la Dini
Husein Juma katika mahafari ya shule ya Sekondari ya Chalinze.
........................
Na Shushu Joel,Chalinze.
VIJANA wengi nchini wamejikuta wakikumbana na changamoto nyingi katika
utafutaji wa maisha katika jamii zao na kupelekea kundi lingine kujiunga katika
matumizi hatari ya utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo hata taifa
kukosa vijana wa kuitumikia serikali yao.
Kukithili kwa vitendo vya uvutaji wa bangi vijiweni kunasababishwa na
wazazi walio wengi kwa kutojenga tabia ya kuwakanya watoto wao pindi wanapokuwa
wadogo na hata inapotokea watoto wao kupewa hadhabu ya viboko na walimu au watu
wengine wazazi wamekuwa wakiwaijua juu wale waliojitokeza kuwakanya watoto hao.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chalinze katika
mahafari ya shule hiyo mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete amewataka vijana
kutokaa vijiweni na watu walioshindikana kwani watawashawishi vibaya na hata
kuwataka waweze kujiunga katika makundi ambayo si mazuri.
Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakishawishiwa na watu wenye nia mbaya
na vijana ili kuwaona tu na wao wanaharibika kwa kufuata matendo mabaya
wanayoyafanya kwenye mitaa ikiwemo ubakaji,uvutaji wa madawa ya kulevya na hata
kwenye wizi.
Kikwete aliongeza kuwa serikali inawategemea kwa kiasi kikubwa ili muweze
kuja kuisaidia katika Nyanja mbalimbali pindi mtakapokuwa wakubwa kwani uongozi
ni mchezo wa kupokezana.
“Mimi mbunge wenu nawahakikishieni serikali ya awamu ya tano imekuwa
imejiwekea mikakati mikubwa ya kuhakikisha vijana wote wanamaliza masomo yao na
wanafaulu ni lazima waende shule bila cha kusingizia kukosekana kwa ada,hivyo
nawatakeni wanafunzi wote katika jimbo la chalinze kuhakikisha kila mmoja wenu
anafaulu ili kuja baadae kuisaidia serikali na Taifa kwa ujumla.
“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imrvutakila
aina ya michango mashuleni kwa madhumuni ya kuona watoto wanapata elimu ya
kutosha pia kuongeza ufaulu kwa watoto” Alisema Kikwete.
Shaabani Husein ni mmoja wa wahitimu katika shule hiyo alisema kuwa
anampongeza mbunge wa jimbo hilo kwa mchango mkubwa anaoufanya kwa vijana wa
shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanasoma kwa bidii bila matatizo ya
aina yeyote ile.
Aliongeza kuwa ushauri uliotolewa ni mkubwa sana hivyo tunamuhakikishia
mbunge kuwa hakuna kijana atakaye potea katika na kujiingiza katika mambo
maovu ya uvutaji wa bangi,wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na
wengi wetu kutambua madhara yake.
Aidha alisema kuwa wazazi walio wengi wamekuwa wakichangia watoto
kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na kutokutumia muda
wao wa ziada kutuelimisha majumbani kwetu na badala yake kazi kubwa kuwaachia
walimu tu.
Naye Mriamu Patrik alisema kuwa madawa ya kulevya yanachangia kwa kiasi
kikubwa kupoteza nguvu kazi ya vijana wetu ambao mara baada ya kujidunga
madawa hayo ulala tu hivyo kupelekea watu hao kutokuwa na nguvu za kufanya
kwani miili yao uzoefu.
“Nampongeza mbunge Ridhiwani Kikwete kwa ushauri alioutoa kwa vijana juu
ya kutambua jinsi gani ijana na kumhakikishia kuwa vijana hao wa shule hiyo
wanazingatia kila ushuri wa viongozi wao wa dini na wale wa serikali kwani
wanahitaji tuwe kwenye maisha yanayositahili”Alisema
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Emanuel Kahabi amewapongeza
wanafunzi wake wanaotarahiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu kwa
nidhamu kubwa wanayoionyesha shuleni na mitaani hii ni kutokana na ushirikiano
mkubwa uliopo kati ya walimu na wazazi katika kuwajengea watoto hao maisha yao
ya baadae.
Aliongeza kuwa wanafunzi watakao maliza kidato cha nne mwaka ni 307 hivyo
kulingana na vile walivyowaandaa wanatarajia matokeo mazuri yatakayofurahisha
zaidi ya mwaka jana.
Aidha amempongeza mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete kwa misaada
mbalimbali anayoitoa katika shule hiyo kwa lengo la kuhakikisha shule hiyo
inakuwa miongoni mwa shule za kisasa na za kuvutia katika jimbo lake.
“Mbunge wetu katusaidia vitu vingi katika kuhakikisha shule hii inakuwa
ya kipekee kwani katuwesheza komputa,mabati,saruji,mbao na vitu vingine vingi
nab ado anaendelea kutusaidia kweli huyu ni kiongozi wa kipekee sana” Alisema
mkuu wa shule hiyo.
Mbunge
wa Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari
Chalize ambapo alikuwa mgeni rasmi katika mahafari ya shule hiyo.
Mbunge
Ridhiwani Kikwete akimkabidhi Cheti cha ufaulu bora wa somo la Kiswahili
mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Chalinze katika Mahafari
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari wakiwa na nyuso za furaha huku wakimsikiliza mgeni rasmi
katika Mahafari hayo.
No comments:
Post a Comment