Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
wadau wa sekta ya Utalii ambapo aliwahikikishia nia ya serikali kuimarisha
ulinzi maeneo yanayotumika kwa shughuli za utalii lengo ikiwa ni kuongeza
mapato kwa nchi na kutumia fursa zinazopatikana katika sekta hiyo.
Kikao
hicho kimefanyika Katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani
Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
............................................
Serikali imedhamiria kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya utalii
kwa kuweka vituo vya polisi vinavyohamishika ikiwa ni mpango wa kuwawekea
mazingira salama wadau wa sekta hiyo na kuongeza mapato kwa nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi
Hamad Masauni, wakati akizungumza na Wadau wa Sekta ya Utalii katika Ukumbi wa
Sheikh Idrisa AbdulWakil, visiwani Zanzibar.
Alisema Serikali inatambua mchango wa sekta ya utalii na inajiandaa
kuweka mipango madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo katika maeneo
yote ya utalii.
“Tunatambua fursa na maendeleo yanayoletwa na utalii na jinsi pato la
nchi litakavyoweza kuongezeka kwa kuimarisha sekta hiyo, hivyo serikali
inakusudia kuweka vituo vya polisi katika maeneo ya utalii huku polisi
wakishirikiana na polisi jamii waweze kuimarisha ulinzi kwa wageni wetu hawa,”
alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa utalii Visiwani Zanzibar, Abdallah
Mwinyi aliiomba serikali kuwafundisha askari polisi elimu ya kumuhudumia mteja
ili waweze kuwahudumia watalii hao pindi wakiwa nchini kwa shughuli za utalii.
“Tunaomba askari wetu wafundishwe elimu ya kuwahudumia watalii ikiwepo
ukaguzi wa magari na watalii pindi wakiwa katika shughuli zao za kitalii lakini
nawapongeza katika kupunguza matendo ya kihalifu katika maeneo kadhaa
wanakopita watalii,” alisema.
Mdau
wa Sekta ya Utalii, Abdallah Mwinyi akizungumza wakati wa
Kikao cha wadau wa sekta hiyo, kilichoitishwa na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, lengo ikiwa ni kusikiliza
changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za utalii. Kikao hicho
kimefanyika Katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani
Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Saleh Mohamed Saleh, akijibu
maswali ya wadau wa utalii yaliyoelekezwa katika idara yake kuhusu
utaratibu wa polisi wa usalama barabarani katika kukagua magari
yanayobeba watalii. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Sheikh
Idrissa Abdul Wakil, visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
Naibu
Kamishna wa Uhamiaji, (D.C.I.) Ali Nassor , akijibu
maswali ya wadau wa utalii yaliyoelekezwa katika idara yake
kuhusu utaratibu wa kuingia nchini kwa watalii. Kikao hicho kimefanyika
katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, visiwani Zanzibar. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment