Tuesday, October 30, 2018

KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA MPANGO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA CHATEMBELEA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA

Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo na Msimamizi wa Mradi wa kukarabati baadhi ya maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Dodoma  Kutoka NHC Bw.Hassan Bendera wakati wa ziara hiyo.

Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akizungumza jambo na Msimamizi wa Mradi wa ukarabati wa baadhi ya maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Dodoma Kutoka NHC Bw.Hassan Bendera walipotembelea kuangalia ukarabati huo, Oktoba 29, 2018.

 
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha nyumba zilizovunjwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege Dodoma wakati walipotembelea kuona hali halisi ya kazi ya upanuzi wa eneo hilo inavyoendelea.
 Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege Dodoma Bi.Bertha Bankwa akitoa maelezo kuhusu upanuzi wa sehemu ya Ukumbi wa abiria wanaoondoka (departure waiting Lounge) kwa Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe walipotembelea ili kuona kazi za upanuzi zinavyoendelea uwanjani hapo.

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege Dodoma Bi.Bertha Bankwa akitoa maelezo kuhusu ukarabati  unaoendelea katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa kikosi kazi cha kuratibu mpango wa  Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea Oktoba 29, 2018.

Mhandisi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Dickson Mmbando akitoa ufafanuzi kwa Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe walipotembelea kukagua upanuzi wa baadhi ya maeneo katika Uwanja huo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment