MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt.
Shukuru Kawambwa akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Amani kata ya Kerege jimboni kwake.
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Amani kata ya Kerege jimboni kwake.
..........................................................
Na Omary Mngindo, Kerege Bagamoyo.
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt.
Shukuru Kawambwa, amesema kuwa Serikali inaendele kuboresha miundombinu ya
barabara, hali inayowezesha watu kusafiri kila kona ya nchi pasipokulala
njiani.
Dkt. Kawambwa ametoa kauli hiyo Kitongoji cha
Amani, Kata ya Kerege akizungumza na wananchi kwenye ziara yake ya kikazi,
lengo kupokea changamoto kisha kuziwasilisha bungeni kwenye kikao kitachoanza
mwanzoni mwa mwezi Novemba.
Kauli ya Dkt. Kawambwa imekuja baada ya mkazi Issa
Ally kulalamikia miundombinu ya barabara, ambapo hata hivyo mkazi mwingine
Kassimu Juma aliishukuru serikali kwa jitiihada inazozionesha katika sekta
hiyo, huku akisema hali ya sasa tofauti na awali.
"Kwa sasa tunashukuru hali ya barabara yetu
sio kama ilivyokuwa hapo awali, angalau inapitika, tunaishukuru Serikali
isipokuwa iongeze bidii ituwekee kokoto ili iwe nzuri zaidi," alisema
Juma.
Akizungumzia barabara, Dkt. Kawambwa alisema kwamba
serikali inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika vijiii na
vitongoji vyote ili ziwe na ubora wakati wote.
"Serikali yenu inaendelea na juhudi za
uboreshani wa miundombinu, hivi sasa hakuna abiria anayelala njiani kwa ajili
ya shida ya usafiri, labda apende mwenyewe, barabara za ndani na kwenda nje ya
nchi zinapitika vizuri wakati wote," alisema Dkt. Kawambwa.
Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Idd
Idd alilalamikia umeme akisema waliahidiwa umeme kupitia Mradi wa usambazaji
umeme vijijini (REA), kwa sasa tunashuhudia
mafundi wa Tanesco wakisimika nguzo kinyume cha taarifa waliyopewa awali.
Dkt. Kawambwa alisema kuwa aliorodhesha vijiji na
vitongoji vyote wakati wa Sospeter Muhongo, akahakikishiwa vitapatiwa umeme
huo, lakini pamoja na yeye kutokuwepo, ufinyu wa fedha umesababisha kutotimizwa
kwa ahadi hiyo.
"Tuendelee kuiunga mkono Serikali yetu ya
awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inavyoendeleza yaliyoachwa na
waliotangulia, katika kuhakikisha tatizo la umeme linabaki historia, kuna mradi
mkubwa wa umeme wa Maporomoko ya maji Mto Rufiji," alisema Mbunge hiyo.
Wananchi wa Kitongoji cha Amani kata ya Kerege
wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa alipofanya
ziara katika kata hiyo.
Madiwani wa viti maalum wakimsikiliza Mbunge,
kulia ni Shumina Rashidi na kushoto ni Togo Omari Hega.
Picha zote na Omary Mngindo.
Picha zote na Omary Mngindo.
No comments:
Post a Comment