MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo, mkoani Pwani, Dk.Shukuru Kawambwa.
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO.
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo, mkoani Pwani, Dk.Shukuru Kawambwa, amewatoa
hofu wananchi watakaopaswa kupisha ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia
Makofia -Mlandizi kwa kiwango cha lami kuwa watalipwa fidia utekelezaji
utakapoanza.
Aidha amewaeleza, wakala wa barabara (TANROADS) bado haijawa tayari
katika utekelezaji huo lakini wale wanaopitiwa na bomba kuu linaloelekea
Bagamoyo ,kuanzia eneo la Sunguvuni -Sanzale watarajie kulipwa fidia zao na
DAWASA hivi karibuni .
Akitolea ufafanuzi suala hilo kwa wakazi wa Chasimba na Magoza, kata ya
Yombo wakati wa ziara yake ya kata kwa kata, Kawambwa alisema walengwa
wanaoguswa na miradi hiyo wavute subira.
Aidha alieleza, ahadi ya malipo ambayo DAWASA italipa anaendelea
kufuatilia ili kupata taarifa zaidi ya malipo hayo .
“Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali, hii
barabara nayo ipo katika utekelezaji wa ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi, “
“Tanroads na DAWASA wamekubaliana wakati ikisubiriwa kufikia ujenzi
wa barabara hiyo, imeingiliana na mradi wa bomba kuu la maji ambapo
DAWASA italipa wale watakaopitiwa na ujenzi huo “alifafanua
Kawambwa.
Kuhusu barabara ya Yombo-Kiegea ,mbunge huyo alisema inatafutwa fedha ili
iweze kuboreshwa kwa kiwango cha changalawe .
“Kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 TARURA haina fedha hivyo kwasasa ni
matengenezo madogo madogo wakisubiri utengenezaji mkubwa baadae endapo kukipatikana
fedha”alibainisha .
Akijibu suala la ukosefu wa umeme huko Chasimba na
Magoza alisema maeneo hayo yameingizwa katika mradi wa Peri Urban na mkandarasi
atakapopatikana watarajie kunufaika na mradi huo mpya.
Awali wakazi wa Chasimba, Magoza kata ya Yombo walisikitishwa umeme
kuwekwa mijini na vijiji kusahaulika kwa miaka mingi.
Walisema ,wanatumia solar kila siku kwa gharama ya sh.3,000, gharama
ambayo ni kubwa kwao kwa maisha ya sasa .
No comments:
Post a Comment