Mama
Salma Kikwete akizungumza katika mahafali ya Shule ya Sekondari Mandera, kulia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Ramadhani Kabelwa na kushoto ni Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Rose Umila.
............................................
Na Omary
Mngindo, Chalinze.
MKE wa
Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne Mama Salma Kikwete, amefurahishwa na
wanafunzi wasichana 49 waliomaliza elimu ya kidato cha nne katika shule
sekondari ya Mandera, Kata ya Mandera, Halmashauri ya Chalinze wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani.
Alisema
amefurahishwa na wasichana hao ambao wanamaliza sfari yao ya masomo bila ya
kuwa na mimba hata mmoja.
Furaha ya
Mama Salma ameitoa kwenye Mahafali ya saba shuleni hapo, ambapo alipoongozana
na Mbunge mwenzake Hawa Ghasia wakiwa na mwenyeji wao Mwalimu Mkuu Rose Umila,
huku akichukizwa na baadhi ya wazazi kutowalipia michango ya chakula watoto
wao.
Alisema
kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipotangaza
elimu bure, alimaanisha hakutokuwepo na ada, na sio kwa huduma za mavazi na
chakula awapo shuleni, na kwamba masuala hayo yanamhusu mzazi na mlezi
mwenyewe.
Katika
Mahafali hayo Mama Salma ambaye pia ni mlezi, amesimamia harambee iliyokusanya
kiasi cha shilingi milioni 1,510,000, mwenyewe akichangia shilingi laki tano
wakati Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akituma laki moja kupitia Mohamed
Mzimba, ambapo Mama Salma aliwaomba wazazi kuhakikisha wanasimamia elimu kwa
mtoto wa kike.
"Nimesikitishwa
na taarifa ya Mwalimu Mkuu inayoeleza kuchelewa kwa baadhi ya wanafunzi baada
ya likizo, sababu zikielezwa kipato kidogo cha wazazi, hali hii inakwamisha
jihudi za mwalimu katika kufundisha, huku mwanafunzi kukosa kile
alicholikikusudia," alisema Mama Salma.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Ramadhani Kabelwa aliwataka wazazi na
walezi kila mmoja aone umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike, huku akiongeza
kwamba kumsomesha mtoto wa kike ni sawa na kuielimisha jamii.
Taarifa ya
Mwalimu Mkuu Umila ameeleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa,
ikiwemo ya uchakavu wa miundombinu shuleni hapo, sanjali na ukosefu wa mabweni
pamoja na bwalo la chakula.
"Tunaishukuru
halmashauri ya Chalinze kwa kutujengea tenki la maji, limesaidia kupunguza adha
hiyo, pia Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu kwa mataulo ya vijana wetu,
sanjali na kikosi cha Jeshi Kiangaiko kinasaidia mambo kadhaa," ilieleza
sehemu ya taarifa ya Umila.
Mama Salma Kikwete akizungumza katika mahafali ya
Shule ya Sekondari Mandera, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,
Ramadhani Kabelwa na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rose Umila.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rose Umila akisoma
taarifa mbele ya mgeni Rasmi, Mama Salma Kikwete.
Mama Salma Kikwete akipokea Taarifa kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rose Umila
Mama Salma Kikweteakimkabidhi saa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rose Umila.
Diwani wa kata ya Mandera Madaraka Mbode wa kwanza kushoto.
No comments:
Post a Comment