Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ameunda kamati ya watu
17 watakaofanya operesheni kabambe ya kuwafundisha adabu watu wanaofanya
ushoga, nyumba zinazotumika kurekodi video za Ngono, wanaojiuza na matapeli wa
njia ya mitandao.
RC Makonda amesema kamati hiyo inajumuisha maafisa wa Polis, TCRA,
Wanasheria, Bodi ya Filamu, Madaktari na Wataalamu wa ushauri na Saha ambapo
kamati hiyo itaanza zoezi la kamatakamata jumatatu.
Operesheni hiyo imepokelewa kwa mikono miwili na mamilioni ya wananchi
ambao wamekuwa wakichukizwa na mmomonyoko wa maadili ambapo RC Makonda hadi
sasa amepokea SMS zaidi ya 18,000 za watu wanaopongeza na kutaja majina ya watu
wanaofanya matendo maovu ikiwemo ushoga na biashara ya ngono.
Aidha RC Makonda amesema hadi sasa amepokea majina zaidi ya 200 ya
mashoga waliotajwa wakiwemo kina James Delicious, Dida Mtamu,Abas,Aunt Miliki
na kundi la Pachupachu.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema oparesheni hiyo pia itahusisha sehemu
za Masaji ambazo baaadhi yake zimekuwa zikijihusisha na biashara ya ngono.
Hata hivyo RC Makonda amesema kuwa hata wanaume watakaotajwa kuwa na
mahusiano ya kimapenzi (wateja) wa Mashoga watakamatwa na kuchukuliwa hatua
Kali za kisheria kwa mujibu wa Sheria.
Sanjari na hayo RC Makonda ametoa angalizo kwa watu wenye picha na video
za ngono kwenye simu zao kuwa operesheni hii haitowaacha salama.
No comments:
Post a Comment