Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani
Kikwete akikagua Gwaride la Jeshi la akiba Chalinze.
Na Shushu Joel,Chalinze.
JESHI la akiba limekuwa ni msaada mkubwa katika jamii ya tanzania
kutokana na vijana wengi wanaojiunga na jeshi hilo punde tu wanapomaliza mafunzo
hayo hupelekea kuwa ni kichocheo kikubwa katika jamii juu ya suala zima la
ulinzi na usalama sehemu wanazotoka vijana hao.
Katika jimbo la chalinze mkoani Pwani wahitimu zaidi 400 wanatarajiwa
kumaliza mafunzo ya Jeshi la akiba mwezi ujao na hivyo kujifungulia fursa kwa
upataji wa ajira kwavijana hao kupitia kwenye mashirika mbalimbali katika
wilaya hiyo ya Bagamoyo.
Wakizungumza na mbunge wao vijana walitaja changamoto zinazowakabili kuwa
ni wengi wao kushindwa kumudu gharama za ununuzi wa kombati mara baada ya
mafunzo ya jeshi la akiba kumalizika kutokana na walio wengi kuonekana ni watoto
yatima.
Kurusumu Shabani ni mmoja wa wanamafunzo wa jeshi la akiba alisema kuwa
wanampongeza mbunge huyo kwa kuwanunulia jeshi la akiba kombati ambazo
watazitumia siku ya mwisho ya mafunzo yao.
Aliongeza kuiwa ni mafunzo mengi yamefanyika hapa nchini lakini viongozi
wachache wenye kuwathamini wahitimu hao kama moja ya sehemu za ulinzi katika
jamii, hivyo Kikwete ni kiongozi wa kuigwa katika jamii.
Aidha alisema kuwa vijana walio wengi katika halmashauri ya chalinze
wameitikia wito wa kujiunga kwenye jeshi la akiba kutokana na utitili wa
viwanda kwenye halmashauri hiyo hivyo ajira za aina nyingi zitapatikana bila
wasiwasi kwa kupitia mafunzo hayo.
Naye Yusuph Mchaga amempongeza mbunge huyo kwa kitendo chake cha
kuwanunulia vijana wa jeshi la akiba kombati hivyo wamemuhakikishia kulinda na
kuzingatia yale yote wanayofundishwa na wakufunzi wao.
Aidha amemuomba mbunge huyo kuwataka wawekezaji wote katika jimbo la
chalinze kuhakikisha wanawapatia kipaumbele vijana wa maeneo hayo na hasa
waliomaliza mafunzo ya jeshi la akiba kutokana na kuwa vijana wanaomaliza
mafunzo hayo huwa na nidhamu ya hali ya juu kutokana na wakufunzi wanawafundisha
kujitolea kutoa misaada mbalimbali katika jamii.
Kutokana na kuwepo kwa mafunzo hayo,mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani
Kikwete amewatembelea vijana hao wanaopata mafunzo ya jeshi la akiba na kutaka
kutatua changamoto zinazowakabili ili waweze kupata vyeti vyao vya kuhitimu
mafunzo yao ya kijeshi.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli
imewafungulia milango ya kutosha vijana kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana
nchini kwa kuwapatia vijana nafasi za kutosha ili wanufaike na nchi yao.
“Vijana wenzangu onyesheni uzalendo wa dhati katika taifa hili kwa
kulitumikia kwa kulinda raia na mali zake pindi mmalizapo mafunzo hayo
mkaisaidie jamii katika masuala ya kutokomeza wizi”Alisema Kikwete.
Aliongeza kuwa kutokan na maombi yenu ya kuniomba kuwasaidia kuwanunulia
kombati nimekubali na nitawanunulia wote ili siku ya mwisho wa kuhitimu mafunzo
yuenu kila mmoja aweze kuwa katika muonekano sahihi wa jeshi la akiba.
Aidha mbunge huyo amewahakikishia vijana hao kuwa pindi watakapo maliza
mafunzo hayo ni lazima setrikali itawaangalia kwa jisho la tatu ili kuhakikisha
wanapatiwa ajira katika sehemu mbalimbali ili iwe fundisho kwa kwa wale wenye
tabia za kubeza mafunzo hayo.
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Sebastian Juma amemponga mbunge huyo kwa
kufika katika mafunzo hayo na kujionea mafunzo hayo jinsi yanavyoendesha kwa
vijana hao.
Aidha amewataka vijana hao kuzingatia mafunzo na kujituma ili kumaliza
wote wakiwa salama kwani lengo la jeshi la akiba ni kuimalisha ulinzi katika
jamii.
No comments:
Post a Comment